ZA UKWELI SANA

WATANZANI TUMWACHE RAISI MAGUFULI AFANYE KAZI YAKE

wabongo tuache tabia ya kulalamika na tumwache mheshimiwa raisi afanye kazi yake tuwache kulalamika,katika awamu iliyopita watanzania wengi walionekana kukerwa na hali ya nchi jinsi ilivyokuwa utendaji mbovu wa wawakilishi wa wananchi na pia,suala zima la ufisadi na wengi walitoa mapendekezo ya aina ya kiongozi waliokuwa wanamtaka,wengi walidai mafisadi hawashughulikiwi na raisi aliyepita hakuwa mkali,mungu si athumani amepatikana ndugu magufuli na ameanza kuonyesha kutenda kazi yake lakini baadhi ya wananchi wameanza kulalamikia speed yake,jamani naombeni tumwache mheshimiwa afanye kazi yake tuwache kulalamika mheshimiwa ni mtu sahihi kabisa tumpe nafasi na muda wa kutenda kazi yake zama za rushwa,ufisadi na kujuana zimepita HAPA KAZI TU.
     MAONI YA MHARIRI. .

MZEE YUSSUFU WA JAHAZI ALIA NA WAKEZE





mwanamuziki wa miondoko ya taarabu nchini,mzee yussufu ameeleza masikitiko yake kwa wake zake wawili ambao amedai hawaivi chungu kimoja,mzee yusufu ameeleza hayo kupitia kipindi cha amplifaya cha clouds fm jana jumatano"hawapatani kabisa nimejaribu kuwasuluhisha lakini imeshindikana,kuna kipindi nijaribu kuwasuluhisha nikawakutanisha kwa pamoja bila wao kujuwa lakini walishindwa hata kusalimiana,natamani waishi kama ndugu lakini imekuwa ngumu,nawaombea sana kwa mungu'alisema mze,wa kwanza nimeishi naye kwa miaka 12,na mwengine kwa miaka 9

DAVIDO ASAINI DILI NA KAMPUNI KUBWA YA MUZIKI DUNIANI SONY ENTERNMENT

Msanii wa muziki kutoka nchini nigeria Davido ameingia kwenye headlines duniani baada ya kuingia mkataba na kampuni kubwa ya muziki duniani ijulikanayo kama sony music enterternment,tukio hilo kibongo bongo huwenda likazima ndoto za wasanii wengi wa kibongo waliotaka kufanya naye collabo ikiwa ni pamoja na allykiba na johmakin kollabo hizo ambazo alizitaja yeye mwenyewe davido,davido ndiye msanii wa kwanza afrika kuingia mkataba na kampuni hiyo.

WEMA SEPETU ADAIWA KUWA MJAMZITO

aliyekuwa mshindi wa shindano la miss Tanzania mwaka 2006 na pia muigizaji wa kike maarufu na anayependwa sana bongo,madam wema sepetu anadaiwa kuwa mjamzito licha ya kusemekana kwamba ni mgumba hana uwezo wa kupata mtoto,kwa mujibu wa jamaa anayesemekana kuwa anatoka naye kwa sasa mshindi wa big brother 2015 idriss sultan ambaye ameonekana kuwa naye karibu kwa hivi sasa.

Idriss amepost picha yake na madam sepetu kupitia mtandao wake wa instagram huku akieleza hisia zake za kimapenzi kwa msanii huyo,huku hakusita kubainisha suala hilo la ujauzito wake.

NANI ZAIDI KATI YA RAPPER 50 CENT NA MEEK MEEL!


marapa wawili kutoka katika kiwanda cha hiphop,meek mill na rapa 50 cent wameingia katika beef rasmi baada ya kuonekana kutupiana madongo na kuandikiana distracks relix kwenye akaunt zao za insta,ikumbukwe pia meek anafanya mpango wa kuingiza albam yake sokoni,huo unaweza ukawa mpango wa kumuingizia mkwanja zaidi rappa huyo.

MWANAMKE MMOJA AKUTWA KWENYE PAA LA JENGO LA WIZARA YA FEDHA

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa haraka,ameonekana kupanda juu la paa la wizara ya fedha,vyanzo vyetu vilipotaka kujuwa kulikoni vilishindwa kupata maelezo ya mama huyo vizuri kutokana na watu waliokuwa wakimzonga zonga mama huyo.

KUMENUKA HUKO INSTAGRAM WEMA ZARRY,NA TEAM ZAO WACHAFUA HALI YA HEWA!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida zarry the boss lady na wema sepetu wamerushiana maneno ya juu,kwa juu huku wakipigana vijembe na kupeana madongo kupitia akaunti zao,hali hiyo ilisababishwa na chokochoko za team zao yaani team  zarry na team wema.

BARNABA CLASSIC,AKARIBISHA WAWEKEZAJI HIGH TABLE SOUND

Mmiliki wa studio ya high table sound barnaba boy ambaye pia ni mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki (producer* amesema anakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kufanya naye biashara ya muziki,barnaba amesema kwa sasa ana wasanii watano kwenye lebo yake amesema anataka kuwekeza nguvu zake nyingi katika kuwasaidia wasanii hao,najua....kumsaidia mwanamuziki mpaka afikie levo kubwa inahitaji pesa nyingi ndio maana nakaribisha wawekezaji ili tuweze kufanya nao kazi na atakaye wekeza na sisi atapata faidakubwa kwa sababu wasanii wote ni wakali alisema barnaba boy,alipoulizwa kuhusu video yake mpya aliyofanya na cameleone anasema ataanza kuachia kwanza audio yake mpya kabla ya kuachia video yake

     KWA HABARI ZAIDI BONGO5.COM

HAA KUMBE HAWA HATA VIJIJINI WAPOOO KUTANA NA BODY BUILDER WAKUKATA NA SHOKA.

Anaitwa abdalah sabuni kutoka wilaya ya muheza kata ya majengo,mkoani Tanga jamaa huyu ana body ya kukata na shoka licha ya kuwa hana gym yenye vifaa vya kisasa lakini amejitengenezea gym mahala anapoishi ambapo ni kwenye nyumba ya kaka yake ambaye anaishi mjini moshi lakini amemkabidhi abdalah sabuni aishi humo,abdalah ametengeneza vifaa vyake mwenyewe vya gym ambavyo vinamsaidia yeye na vijana wengine wanaopenda mazoezi na humlipa abdalah ujira wa sh..miatano kila siku,ambayo bwana abdalah amesema humsaidia kujikim kwenye masuala yake muhimu,licha ya kuwa body builder abdalah amesema yeye ana  vipaji vingi tofauti na body building kwani anaimba muziki wa hiphop,anafanya karate na mengine mengi,Adlah sabuni ana ndoto za kutoboa kwenye muziki wa hiphop lakini anakwamisha na fedha za kwenda kurekodia tu,.....nimeshafanya kazi nyingi kwenye studio ndogo ndogo za hapa tanga...na kushinda  mashindano ya muziki hapa wilayani muheza mara kadhaa.....anaelezea abdalah sabuni almaarfu kama DSAB,kwa sasa dsab shughuli yake kuu inayompa riziki ni kuchonga mihuri....kwa yeyote atakayeguswa na kumsaidia kijana huyu katika kazi zake za sanaa awasiliane nasi kupitia namba 0656538476.

UZURI WA MWANAMKE NI SURA NA TABIA PIA!

kuna maneno mengi ya mitaani kuhusu kitu gani cha kutazama wakati wa kumtafuta mwanamke wengine husema mwanamke ni tabia,wengine husema ni uzuri na wengine husema vyote vinahusika mimi kama mwandishi nasema mwanamke lazima awe na uzuri wa kiasi cha kumridhisha mwenzi wake na tabia njema pia ni muhimu,ifahamike kwamba kila mtu ana kipimo chake cha uzuri kwa ampendae mzuri kwako anaweza kuwa mbaya kwa mwengine kwa hiyo hilo linategemea na mtu mwenyewe,.....ila vyote ni muhimu je wewe msomaji nini maoni yako?tuandikie hapo chini maoni yako

TAZAMA HILI KANISA LILILOJENGWA KWA MFANO WA KIATU CHA MWANAMKE*HIGH HEELS* HUKO TAIWAN

Hili ni kanisa ambalo,limetengenezwa spesho kwa ajili ya kuwavutia wanawake,lipo huko nchini Taiwani kiongozi wa kanisa hilo amesema kuwa kanisa hilo halitatumika kwa ibada za kawaida bali litatumika kwa shughuli za harusi zaidi.

MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHUKIA WABONGO WANAOMSEMA ANATAFUTWA NA TRA.

Msanii wa vichekesho kutoka kampuni ya orijino komedi,inayowaunganisha wenziwe watano mpoki,joti,vengu,makregan na wakuvwanga leo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na kipindi cha clouds 360,kinachorushwa na clouds tv asubuhi,alipoulizwa kuhusiana na gari yake ya mac x kwamba anatafutwa na TRA kwamba hajalipia mapato amesema....si kweli na kwamba magari yake yote anayomiliki na mali zake zipo wazi kiasi ambacho hata mwenyekiti wa kijiji anazijua.....nini macx nina vitu vingi vinavyoweza kununua mac x nyingi sio moja tu..mimi nguvu zangu nyingi zipo kwenye kilimo,wabongo wengi ni wavivu wanataka tu kukaa na kutumia mitandao ya kijamii hawataki kufanya kazi,,,,,ndio maana mtu anapofanikiwa kidogo hukimbilia kusema jambo la kwanza ni muuza unga tu alisema mkandamizaji!......alipoulizwa kuhusu safari zake za mara kwa mara za marekani amesema yeye ni street pastor au mchungaji wa mitaani kwa hiyo anachofuata kule ni suala la kuhubiri injili tu na si kitu kingine na kwamba ameshakwenda nchi nyingi tu kama norway,na uingereza mbali na nchi ya marekani ambayo amekwenda mara kwa mara,alibainisha mkandamizaji mapema leo.
kama TRA wananitafuta mwanawani nipo hapa clouds tv live waje wanikamate nipo hapa live na chombo kipo hapo bondeni tu...akimaanisha amekuja nalo gari lake linalohusishwa na utata huo katika studio hizo za clouds tv.

WABONGO TUACHE ROHO ZA KWA NINI SI UTAMADUNI WETU!

Asalam aleikum watanzania wenzangu wote mnaosoma ujumbe huu,leo napenda niwakumbushe watanzania wenzangu asili yetu kidogo maana kadiri siku zinavyokwenda utandawazi unavyozidi kuchukuwa nafasi na hali za kiuchumi zinavyowabana watu basi ndivyo roho za mtanzania wa leo zinavyozidi kubadilika kutoka kwenye ubinaadamu kwenda kwenye unyama,ni rahisi sana kwa mtanzania wa leo kupelekewa kadi ya mchango wa harusi ya shilingi laki moja,lakini ni ngumu mtanzania huyohuyo kumchangia mtoto aliyekosa ada shilingi elfu ishrini akapate elimu,mara kadhaa tumesikia wasanii wachanga aidha kwenye muziki au filamu hapa bongo,wakiwalalamikia baadhi ya wasanii wenzao ambao wamekwisha tangulia kutoka kisanaa na pengine hata kwa kuwataja majina kabisa kwamba wamekataa kuwapa ushirikiano kabisa mara walipokwenda kuwaomba msaada kwa namna moja au nyingine,na wengine walidiriki hata kuwakatisha tamaa wenzao kabisa kwa kuwaambia waache kabisa sanaa,lakini leo hii wamekuwa wasanii wakubwa pengine hata kuwashinda wao wenyewe,roho mbaya ni uoga na kukosa kujiamini miongoni mwetu.
wakati wenzetu kama nigeria wakipeana sapoti katika masuala ya muziki na filamu sisi kwa ujinga wetu tunaendeleza matimu ya kipuuzi,sikatai kwamba nchi za wenzetu hakuna timu hapana lakini wenzetu wapo kikazi zaidi,roho mbaya na za kwanini haijaishia hapo tu hata kwa bloggers wa kitanzania pia zipo roho za kwanini wakati fulani wakati nataka kuanzisha blogs zangu niliwafikia baadhi ya bloggers wa muda mrefu na pia niliona kuwa ni wazoefu lakini kwa kweli hawakuonyesha ushirikiano kwa kweli......mara wanakwambia maudhui yanafanana na wenzako wakati yeye mwenyewe anaandika taarifa za habari na blogs nyingi tu maarufu nazo zinaandika taarifa za habari,kwa hiyo unapata majibu ni mtu asiyetaka kukupa msaada hivyo anatafuta tu vijisababu.
wabongo tuache ubinafsi,ni roho ya uwoga na kutojiamini bloggers wenzangu wake up,roho za kimaskini hizo jiamini unachokifanya hakuna zaidi yako kama wewe hakuna anayeweza kufanya kama wewe,mtanzania ni mkarimu na mwenye upendo,hata taifa letu linasifiwa nje ya nchi kwa upendo na ukarimu,taifa letu pia lilisaidia nchi nyingi kupata uhuru wao,mbona sisi wenyewe hatupendani?.......halafu ndio wa kwanza kulalamika kwamba taifa letu haliendelei litaendelea vipi wakati hatupeani sapoti?hatupendani....kizuri ufanye wewe tu kibaya wafanye wenzako.
        

KULIKONI MABINTI WENGI KUPENDA PIPI ZA VIJITI *LOLIPOP*

Add captionKumekuwa na mtindo kwa mabinti wengi bongo na pengine hata nje ya bongo mabinti wengi hupenda kupiga picha au kumingo kwa mitaa na pipi za vijiti maarufu kama lolipop,huku wakiweka mapozi tofauti tofauti je kulikoni,kuna uhusiano gani kati ya wadada na pipi za vijiti swagz,style,au vifuata upepo tu?usisite kutuandikia maoni yako hapa tupate kujifunza zaidi karibuni nyooote mtiririke hapa!

USO WA KAZI

USO WA KAZI MWAKA WA KAZI 2016 HAPA KAZI TU

ELIMU BURE YA MAGUFULI WAZAZI WAELIMISHWE

Kumekuwepo na sintofahamu nyingi kwa baadhi ya wazazi hapa nchini katika utekelezwaji wa agizo la mheshimiwa magufuli ikiwa ni moja kati ya ahadi zake wakati wa kampeni,mapema tu mwaka uliopita moja ya ahadi ambayo imeleta sintofahamu kwa baadhi ya wazazi hasa kwa kipindi hiki shule zinapokwenda kufunguliwa ni pamoja na ile ya elimu bure yaani pasipokuwa na malipo ya ada kwa shule za msingi na sekondari za serikali,suala hilo limeleta utata mkubwa kwa baadhi ya wazazi kwani wengine wamegoma kuwanunulia watoto wao hata mahitaji muhimu  kama sare za shule madaftari na kalamu,huku wakidhani kwamba suala hilo ni la serikali ya raisi magufuli
bado watanzania wengi wapo gizani kuhusiana na suala la elimu bure ,hivyo tunawaomba wadau pamoja na serikali kuwafikia wazazi wengi zaidi ili kuwaelimisha ni yepi majukumu ya wazazi na ni yepi majukumu ya serikali kuhusiana na sera ya elimu bure ili vijana wetu wapatiwe elimu iliyo bora.

MADEE AAMUA KUJA NA BIASHARA YA MAGARI

Mwanamuziki Hamadi ally a.k.a madee ameamua kuja na biashara tofauti kidogo baada ya kuamua kuanzisha kampuni ya uuzaji wa magari hapa nchini,madee  amesema yupo mbioni kuanzisha kampuni hiyo mapema mwaka huu baada ya kuona ni nzuri vilevile ina maslahi kwa upande wake.

HARMONIZE AAMUA KUCHORA TATOO YA DIAMOND KAMA ISHARA YA SHUKRANI

Msanii chipukizi wa miondoko ya bongofleva nchini,kutoka katika lebol ya wcb inayomilikiwa na mkali diamond platnumz nasbu abduli,ameamua kuchora tatoo ya picha ya boss wake diamond kama ishara ya kumshukuru kwa kumsaidia kumtoa kimuziki,harmonize aliambatanisha picha na maelezo ya kumshukuru platnamz kupitia mtandao wake wa picha wa instagram,japo mashabiki wake wameonekana wengine wakibeza kwa kusema alipaswa achore tatoo ya wazazi wake na wengine wakimsifia kwa jambo hilo,harmonize ni msanii anayetamba na kibao chake cha aiyola,ambapo aliifanyia video ya wimbo wake nchini s.a harmonize ni msanii chipukizi lakini anaonekana kufanikiwa haraka kutokana na kuwa chini ya manejment ya diamondplatnamz


ZARRY THE BOSS LADY NDANI YA SOUTH AFRICA


MAGAZETINI LEO JUMATATU.