ZA UKWELI SANA

NAMNA YA KUONDOA UWOGA

Mpendwa msomaji wa blogu hii pendwa,nadhani kila mmoja wenu anamfahamu adui huyu aitwaye uwoga,huyu ni adui mbaya sana,lakini kitu cha ajabu,adui huyu tunae kila  tukilala na kila tunapoamka tunakwenda naye makazini na kila sehemu tupo naye,uwoga ni hisia hasi juu ya  mambo fulanifulani lakini cha ajabu adui huyu tuna mtengeneza wenyewe kwenye vichwa vyetu,leo nimekuandalia dondoo chache za namnna unavyoweza kukaa mbali na uwoga  na ukafanya mambo yako kwa amani kabisa,uwoga upo wa vitu vingi kama vile,uwoga wa kifo,uwoga wa kupata shambulio la moyo,uwoga wa kukataliwa,uwoga wa kuongea mbele za watu,uwoga wa kufeli mtihani n.k
ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI ZA KUONDOA  UWOGA;
  1. Jua kitu unachokihofia;wataalamu wa mambo wanasema kumjua adui yako ni njia moja wapo ya kushinda vita,uwoga mara zote unakuwa ni juu ya kitu usichokijua.Usipokijua kitu kinachokukabili vizuri unaweza kuvuta taswira hasi katika kichwa chako,kwa hiyo yakupasa usifikiri vibaya au negative juu ya hilo jambo fikiri juu ya kushinda sio kushindwa,mara nyingi asilimia kubwa ya vitu tunavyofihofia huwa havitokei,na hata madhara yanapotokea hayawi na athari kubwa kama vile tunavyodhani,hutakiwi kuogopa jambo lolote lile zaidi ya kutenda dhambi tu.
  2. FANYA VILE VITU UNAVYOVIHOFIA AU UNAVYOVIOGOPA;usipokuwa tayari kujaribu kufanya mambo unayoyaogopa yataendelea kukutesa mara kwa mara,kwa mfano unaogopa kuzungumza mbele za watu,inabidi uanze taratibu kujifunza mpaka uzoee,haijalishi unaogopa kwa kiasi gani,kama mtu unaogopa kupanda ndege inabidi ujitoe muhanga na ujaribu kufanya hivyo,kwani mtu aliyezoea kupanda ndege mara kwa mara ni tofauti sana na yule anayeanza kwa mara ya kwanza,kadiri unavyozidi kufanya mara kwa mara ndipo unapozidi kuzoea,kama unataka kujifunza kuendesha gari inabidi uanze kujifunza kama unaogopa kujaribu,hutakuja kujua kamwe kuendesha gari,na bila kusahau kadiri unavyozidi kuogopa jambo ndipo linazidi sana kukutesa,ni lazima ili ufanikiwe katika maisha kujitoa muhanga kujaribu na kufanya mpaka tuweze.
  3. MTU AMBAYE HATAKI KUJITOA MHANGA KUJARIBU AU KUFANYA HAWEZI KUJIFUNZA CHOCHOTE MAISHANI MWAKE. 
  4. USIFIKIRIE SANA MAMBO UNAYOYAHOFIA,kama unaogopa wachawi au majini usifikirie sana mambo hayo,fikiria mambo yanayoweza kukupa amani na furaha maishani mwako law of nature inasema kadiri unapozidi kuwaza kitu sana na kukiogopa ndipo kinavyoweza kukuletea madhara sana.
  5. USIJITENGENEZEE MSIBA AU MAJANGA MWENYEWE KATIKA MAISHA;huwezi kuliogopa jambo lolote bila kuiambia nafsi yako au akili yako kwammba hili ni jambo baya,kama utajiambia mwenyewe kwamba hicho unachokiogopa ni kitu cha kawaida na hakiwezi kukuathiri kwa namna yeyote ile,utakisahau na kitapita tu,mwisho kabisa lazima tukumbuke kila jambo katika maisha linatokea kwa mipango ya MUNGU,hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya au kwa ajali tu,mshirikishe MUNGU,kwenye matatizo yako yote nawe utaishi kwa amani sana,MUNGU ndiye mwisho na mwanzo wa yote.



    MSHINDE ADUI UWOGA UISHI KWA AMANI.
  6. THINK POSTIVE GROW RICH. 
     
     THINK BIG.

0 Response to " NAMNA YA KUONDOA UWOGA "

Chapisha Maoni