![]() |
mamy na dady family. |
Neno Dady/mamy hili hutumika miongoni mwa jamii chache sana barani africa,maneno haya humaanisha mzazi wa kike au wa kiume,lakini pia father/mother humaanisha mzazi wa kike na wa kiume miongoni mwa jamii nyingi sana sana za ki africa,japo yanatumika kuleta maana moja lakini yana utofauti mkubwa sana kimaana kama ifuatavyo;
neno mamy/dady haya ni majina ya wazazi wengi waliojiandaa vizuri kutunza na kulea familia zao,mara nyingi watoto katika familia hizi huwa ni wachache na waliozaliwa kimpangilio maalumu,wazazi katika familia hizi huwa ni marafiki sana na watoto,watoto huwapenda sana haswa mzazi wa kiume,husomeshwa katika shule nzuri,hupatiwa mavazi mazuri sana,nyumba za familia hizi hutengewa maeneo mazuri kwa ajili ya michezo,na huwa na vifaa kwa ajili ya kuwaweka sawa kimwili na kiakili pia kama vitenesi,mipira,computer games na wakati mwingine nyumba huwekewa maeneo ya kuogelea maarufu kama swimming pool,katika familia hizi watoto mara zote huwa wasafi kubadilisha vyakula na vinywaji huwa ni jambo la kawaida sana,wakati mwingine pia husaza,mavazi mafupi kwa watoto
wa kike huwa si dhambi wala tabia mbaya bali ni kupendeza na kuleta mvuto pia,familia hugubikwa na upendo furaha na amani ya kutosha mno,na watoto wa familia hizi huwa na uwezo mzuri pia wa kufikiri na kupambanua mambo.
sasa tuangalie hali inakuwaje katika familia ya father/mother mara nyingi familia hizi ndio nyingi sana barani africa,na huwa mpangilio wa watoto mara nyingi huwa ni wengi sana tofauti na uwezo wa familia husika, wazazi katika familia hizi huwa ni maadui wa watoto,haswa wazazi wa kiume,baba anaposafiri katika familia hizi huwa ni sherehe kwa watoto na anapokuwa nyumbani huwa ni huzuni sana,vyakula huwa ni vya aina moja tu,na kunapopikwa vyakula ambavyo ni vizuri au vinavyoonekana kuwa vitamu kunakuwa na tukio maalumu labda sherehe,sikukuu au amekuja mgeni,watoto husoma shule zisizokuwa na elimu bora,watoto wadogo huenda kucheza mbali na nyumbani kwao na hawarudi mpaka watafutwe hurudi wakiwa wamechafuka sana na hupokelewa kwa vipigo vikali sana na kutukanwa matusi mazito kuliko umri wao,kunapopikwa chakula kizuri watoto huenda kufunua masufuria na vyungu vya kupikia na hapo huweza kudokoa chakula kabla ya kuandaliwa mezani,na mara nyingi watoto katika familia hizi huwa na upeo mdogo sana wa kufikiri
kuna baadhi ya waazi wengine wana maisha mazuri sana kama ya dady na mamy family,lakini kutokana na kuathiriwa na maisha ya father na mother walipokuwa wadogo na wao wanataka watoto wao wapitie maisha kama hayo,wakidhani kwamba ndio malezi bora kumbe huwa wanajidanganya wenyewe.
![]() |
father na mother family. |
![]() |
DADY AND MAMY FAMILY WAKIPATA CHAKULA CHA JIONI. |
wazazi kumbukeni kujiandaa kabla ya kutengeneza familia ili kuweza kuwatengenezea watoto wenu maisha bora zaidi
haya ni mawazo binafsi ya mwandishi na utafiti binafsi hayafungamani na upande wowote.
piga simu no 0656538476 kwa maoni na ushauri tu.
0 Response to "HII NDIO TOFAUTI KATI YA DADY/MAMY AND FATHER/MOTHER"
Chapisha Maoni