ZA UKWELI SANA

MAKAHABA NCHINI KENYA WATUMIA PEP KUZUI MAAMBUKIZI YA UKIMWI.

Makahaba nchini ya Kenya wameeleza kwamba hutumia vidonge vya kuzuia maambukizi ya Ukimwi vinavyo julikana kama PEP,kila mara wanapokutana na wateja wao bila kutumia kinga,wameeleza kwamba huenda katika vituo vya Afya nchini humo na kupatiwa vidonge hivyo kwa madai ya kubakwa au mipira ya kufanyia mapenzi kupasuka wakati wa tendo,akizungumza na kituo cha citizen nchini kenya muuguzi mmoja jina kapuni nchini humo ameeleza kwamba matumizi ya vidonge hivyo huzuia kwa asilimia 95 maambukizi ya virusi vya ukimwi.
     amesema kwa kipindi cha mwaka 2013 zaidi ya  watu 1426 wamekwenda kuchukua vidonge hivyo alipoulizwa kama kuna madhara yeyote ya kutumia vidonge hivyo amesema vikitumiwa ipasavyo havina madhara kabisa.
     Makahaba nchini humo wamesema hawana namna ya kuacha kufanya biashara hiyo kwani ndo mahala wanapoweza kupata mahitaji yao muhimu kama ada za watoto,chakula,malazi,kodi za nyumba na mahitaji mengineyo,wameeleza kuwa wakifanya mapenzi bila kinga wanapatiwa pesa nyingi kuliko kutumia kinga.
    je uonavyo wewe hakuna namna ya makahaba kuendesha maisha mpaka wauze miili yao?hakuna ugonjwa mbaya kama uvivu wa kufikiri.

0 Response to "MAKAHABA NCHINI KENYA WATUMIA PEP KUZUI MAAMBUKIZI YA UKIMWI."

Chapisha Maoni