ZA UKWELI SANA

Umasikini Ni Janga La kitaifa.

Katika nchi inayoendelea kama Tanzania yenye takribani vijana asilimia 60 bado hali ya kimaisha kwa vijana wengi ni duni na hili likichangiwa na ukosefu wa ajira mamia ya vijana kila mwaka wamekuwa wakihitimu elimu za juu,vyuo na mashule kila mwaka huku wakiwa hawana ajira hali inayopelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukahaba,uwizi na ujambazi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya.
  Mheshimiwa Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa ameripotiwa akisema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu na siku moja litakuja kulipuka.
    Sisi kama jicho la harakati kitaa tunawaomba vijana wanaohitimu elimu ya vyuo na mashule kuacha kutegemea kuajiriwa na badala yake wawe wabunifu na kuchangamkia fursa zilizopo kwenye jamii zao kwa mfano kuna taasisi zinazotoa mikopo lakini kwa mashariti ya kukaa kwenye vikundi mnaweza kubuni mradi na utekelezaji wake na mkapatiwa mikopo na kubadilisha maisha kabisa tujenge utamaduni wa kujitegemea vijana.
    Kabla ya ukosefu wa mitaji kwa vijana bado tuna matatizo ya mawazo ni kipi unachotakiwa kufanya kwani unaweza kupatiwa fedha na ukashindwa kujiendeleza kabisa.

0 Response to "Umasikini Ni Janga La kitaifa."

Chapisha Maoni