ZA UKWELI SANA

CHUPI YA SHANGAZI

maisha ni matamu sana,lakini wanadamu tunapopitia misukosuko na majaribu mengi katika haya maisha hapa duniani,tunaaona maisha ni kama shubiri,nakuhisi kama mwenye enzinzi mungu,ametutupa na kutusahau kabisa...lakini hakika haya yote ni mapito tu,yaliyonikuta mimi katika dunia hii ni ngumu kusimulia kwani ninapo yakumbuka nahisi kuumiza moyo wangu lakini haya ndio nilioyapitia endelea kufuatilia kisa hiki.
     ilikuwa ni jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi mwaka 1995,alfajiri nikiwa bado nimelala,nikasikia watu wakiteta dirishani kwangu,eeeh....sawa,ataona mimi ni mzee wa mipango bwana....ndio wewe niamini mimi bwana,ilisema sauti  yenye kukwaruza kama mtu aliyeongea kwa muda mrefu na sasa sauti inataka kukauka,lakini ilikuwa sauti ya mwanamume mtu mzima,mara ikajibu sauti ya kike lakini nzito ikisikika kwa kunong'ona .....usiniangushe mtu wangu ohoo....nilichungulia katika dirisha langu dogo kule nje kwa umakini mkubwa,huku kamwanga kajua kakianza kuchomoza na kunipiga usoni,ulikuwa ni msimu wa kiangazi kwa ivyo jua huchomoza mapema sana,kutizama nje ndipo nilipomuona mzee sabanda,mzee ambaye anahusishwa sana na mambo ya kichawi na ushirikina sana pale kijijini kwetu na watu humuogopa sana kama mungu wa pale kijijini,mzee sabanda alikuwa na mwanamke mnene na mfupi mwenye mashavu makubwa na alikuwa ni mweusi mwanamke yule nilikaza macho vizuri kuweza kumtambua mwanamke yule vizuri licha ya mwanga hafifu wa alfajiri kwani walikuwa wamesimama ule upande usichomoza jua,ndipo nilimtambua mwanamke yule kuwa ni bi tatu ally,ambaye ni shangazi yangu,nikajiuliza masuali mengi shangazi huku kafuata nini hasa ukizingatia anaishi kijiji cha tatu kutoka pale kijijini kwetu,huko ndiko alikoolewa na anaishi na familia yake huko....wakati naendelea kutafakari hayo,mzee sabanda aligeuza shingo kisha alikaza jicho,kama aliyekuwa ameona kitu,...nilipatwa na mshtuko nikadhani mzee sabanda atakuwa ameniona hasa ukizingatia mzee huyo hana masihara hata kidogo,na ni mzee hatari sana pale kijijini kwetu,na tangu ni mfahamu mzee huyu maji ya kunde mwenye sauti ya kukwaruza aliyependelea kula ugoro kila mara,sijawahi kumuona akicheka wala kutabasamu hata mara moja na watoto wadogo wamekuwa wakimuogopa sana,Mzee sabanda alikaza jicho kuelekea dirishani kwangu muda wa dakika moja hivi,kisha akavuta pumzi kidogo,alionekana kama aliyekuwa akitafakari jambo,kisha akampa mkono yule mwanamke mwenye mashavu makubwa na sura ya kiume na sauti nzito ya zege,bi tatu ally ambaye nilimfahamu kama shangazi yangu na wote wawili kila mtu alishika njia yake...
     INAENDELEA KESHO USIKOSE.......

PIGA 0656538476
KWA MAONI USHAURI NA MATANGAZO.
 

0 Response to "CHUPI YA SHANGAZI"

Chapisha Maoni