ZA UKWELI SANA

JITOE KATIKA UTUMWA WA KIFIKRA,HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUKUWEKA HURU.

Mara ngapi umejiuliza umuhimu wa hayo mawazo hasi yanayokusumbua,kama uwoga wa kufanya jambo,kukata tamaa na kuwa na imani ya kushindwa maishani mwako?maandiko ya dini yanasema afikiriavyo mtu ndivyo alivyo,mungu anatenda kazi kulingana na fikra na mawazo yetu,na pia vitabu hivyo hasa biblia ukisoma mwanzo inasema mungu amemuumba mwanadamu kwa mfano wake,....hiyo ni habari njema kwetu wanadamu, mungu katika mipango yake hajashindwa,hatashindwa kamwee...na kamwe kabisa.kama mungu hajashindwa na hatashindwa kamwe na sisi wanadamu tumeumbwa kwa mfano wake basi hatuna sababu ya kukata tamaa,na wala kuweka imani ya kushindwa.....ni kujaribu na kujaribu bila kukata tamaa kwa maana agano la mungu kwa wanadamu ni kufanikiwa,na pia ni kushinda kwa maana mungu hajawahi kushindwa,na pia tusifikiri kushindwa,tufikiri ushindi kwa maana mungu anatenda kazi kwa kutumia fikra na mawazo yako kama unafikiria kushindwa,basi utashindwa kama unafikiria kushinda pia utashinda,mtu huvuna kile akipandacho,ukipanda uharibifu utavuna uharibifu,ukipanda mema utavuna mema...hiyo ndio kanuni na fomula ya kimungu na ulimwengu kwa ujumla....maisha ni uchaguzi kuwa masikini,au kuwa tajiri,kuwa na furaha au kuwa na huzuni,maisha yapo kiganjani mwako kwa kutumia fikra na mawazo yako tu.vipi wewe unajichagulia mabaya?una waza mabaya juu yako?au umejikatia kabisa tamaa ya kuishi?hapana unafanya maisha yako kuwa mabaya zaidi kwa mawazo chanya na kadiri unavyojiwazia mabaya ndivyo unavyoyakaribisha kwenye ulimwengu halisi wa kimwili,na pia unavyojiwazia mema ndivyo unavyokaribisha ushindi maishani mwako....kumbuka utavuna ulichopanda katika fikra zako.
   amua sasa kuwa na furaha maishani mwako,think big and grow rich.
  0656538476 tunakaribisha matangazo,na usisite kututumia maoni yako hapa.

0 Response to " JITOE KATIKA UTUMWA WA KIFIKRA,HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUKUWEKA HURU."

Chapisha Maoni