ZA UKWELI SANA

HAA KUMBE HAWA HATA VIJIJINI WAPOOO KUTANA NA BODY BUILDER WAKUKATA NA SHOKA.

Anaitwa abdalah sabuni kutoka wilaya ya muheza kata ya majengo,mkoani Tanga jamaa huyu ana body ya kukata na shoka licha ya kuwa hana gym yenye vifaa vya kisasa lakini amejitengenezea gym mahala anapoishi ambapo ni kwenye nyumba ya kaka yake ambaye anaishi mjini moshi lakini amemkabidhi abdalah sabuni aishi humo,abdalah ametengeneza vifaa vyake mwenyewe vya gym ambavyo vinamsaidia yeye na vijana wengine wanaopenda mazoezi na humlipa abdalah ujira wa sh..miatano kila siku,ambayo bwana abdalah amesema humsaidia kujikim kwenye masuala yake muhimu,licha ya kuwa body builder abdalah amesema yeye ana  vipaji vingi tofauti na body building kwani anaimba muziki wa hiphop,anafanya karate na mengine mengi,Adlah sabuni ana ndoto za kutoboa kwenye muziki wa hiphop lakini anakwamisha na fedha za kwenda kurekodia tu,.....nimeshafanya kazi nyingi kwenye studio ndogo ndogo za hapa tanga...na kushinda  mashindano ya muziki hapa wilayani muheza mara kadhaa.....anaelezea abdalah sabuni almaarfu kama DSAB,kwa sasa dsab shughuli yake kuu inayompa riziki ni kuchonga mihuri....kwa yeyote atakayeguswa na kumsaidia kijana huyu katika kazi zake za sanaa awasiliane nasi kupitia namba 0656538476.

0 Response to "HAA KUMBE HAWA HATA VIJIJINI WAPOOO KUTANA NA BODY BUILDER WAKUKATA NA SHOKA."

Chapisha Maoni