ZA UKWELI SANA

MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHUKIA WABONGO WANAOMSEMA ANATAFUTWA NA TRA.

Msanii wa vichekesho kutoka kampuni ya orijino komedi,inayowaunganisha wenziwe watano mpoki,joti,vengu,makregan na wakuvwanga leo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na kipindi cha clouds 360,kinachorushwa na clouds tv asubuhi,alipoulizwa kuhusiana na gari yake ya mac x kwamba anatafutwa na TRA kwamba hajalipia mapato amesema....si kweli na kwamba magari yake yote anayomiliki na mali zake zipo wazi kiasi ambacho hata mwenyekiti wa kijiji anazijua.....nini macx nina vitu vingi vinavyoweza kununua mac x nyingi sio moja tu..mimi nguvu zangu nyingi zipo kwenye kilimo,wabongo wengi ni wavivu wanataka tu kukaa na kutumia mitandao ya kijamii hawataki kufanya kazi,,,,,ndio maana mtu anapofanikiwa kidogo hukimbilia kusema jambo la kwanza ni muuza unga tu alisema mkandamizaji!......alipoulizwa kuhusu safari zake za mara kwa mara za marekani amesema yeye ni street pastor au mchungaji wa mitaani kwa hiyo anachofuata kule ni suala la kuhubiri injili tu na si kitu kingine na kwamba ameshakwenda nchi nyingi tu kama norway,na uingereza mbali na nchi ya marekani ambayo amekwenda mara kwa mara,alibainisha mkandamizaji mapema leo.
kama TRA wananitafuta mwanawani nipo hapa clouds tv live waje wanikamate nipo hapa live na chombo kipo hapo bondeni tu...akimaanisha amekuja nalo gari lake linalohusishwa na utata huo katika studio hizo za clouds tv.

0 Response to "MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHUKIA WABONGO WANAOMSEMA ANATAFUTWA NA TRA."

Chapisha Maoni