ZA UKWELI SANA

WABONGO TUACHE ROHO ZA KWA NINI SI UTAMADUNI WETU!

Asalam aleikum watanzania wenzangu wote mnaosoma ujumbe huu,leo napenda niwakumbushe watanzania wenzangu asili yetu kidogo maana kadiri siku zinavyokwenda utandawazi unavyozidi kuchukuwa nafasi na hali za kiuchumi zinavyowabana watu basi ndivyo roho za mtanzania wa leo zinavyozidi kubadilika kutoka kwenye ubinaadamu kwenda kwenye unyama,ni rahisi sana kwa mtanzania wa leo kupelekewa kadi ya mchango wa harusi ya shilingi laki moja,lakini ni ngumu mtanzania huyohuyo kumchangia mtoto aliyekosa ada shilingi elfu ishrini akapate elimu,mara kadhaa tumesikia wasanii wachanga aidha kwenye muziki au filamu hapa bongo,wakiwalalamikia baadhi ya wasanii wenzao ambao wamekwisha tangulia kutoka kisanaa na pengine hata kwa kuwataja majina kabisa kwamba wamekataa kuwapa ushirikiano kabisa mara walipokwenda kuwaomba msaada kwa namna moja au nyingine,na wengine walidiriki hata kuwakatisha tamaa wenzao kabisa kwa kuwaambia waache kabisa sanaa,lakini leo hii wamekuwa wasanii wakubwa pengine hata kuwashinda wao wenyewe,roho mbaya ni uoga na kukosa kujiamini miongoni mwetu.
wakati wenzetu kama nigeria wakipeana sapoti katika masuala ya muziki na filamu sisi kwa ujinga wetu tunaendeleza matimu ya kipuuzi,sikatai kwamba nchi za wenzetu hakuna timu hapana lakini wenzetu wapo kikazi zaidi,roho mbaya na za kwanini haijaishia hapo tu hata kwa bloggers wa kitanzania pia zipo roho za kwanini wakati fulani wakati nataka kuanzisha blogs zangu niliwafikia baadhi ya bloggers wa muda mrefu na pia niliona kuwa ni wazoefu lakini kwa kweli hawakuonyesha ushirikiano kwa kweli......mara wanakwambia maudhui yanafanana na wenzako wakati yeye mwenyewe anaandika taarifa za habari na blogs nyingi tu maarufu nazo zinaandika taarifa za habari,kwa hiyo unapata majibu ni mtu asiyetaka kukupa msaada hivyo anatafuta tu vijisababu.
wabongo tuache ubinafsi,ni roho ya uwoga na kutojiamini bloggers wenzangu wake up,roho za kimaskini hizo jiamini unachokifanya hakuna zaidi yako kama wewe hakuna anayeweza kufanya kama wewe,mtanzania ni mkarimu na mwenye upendo,hata taifa letu linasifiwa nje ya nchi kwa upendo na ukarimu,taifa letu pia lilisaidia nchi nyingi kupata uhuru wao,mbona sisi wenyewe hatupendani?.......halafu ndio wa kwanza kulalamika kwamba taifa letu haliendelei litaendelea vipi wakati hatupeani sapoti?hatupendani....kizuri ufanye wewe tu kibaya wafanye wenzako.
        

0 Response to "WABONGO TUACHE ROHO ZA KWA NINI SI UTAMADUNI WETU!"

Chapisha Maoni