ZA UKWELI SANA

ELIMU BURE YA MAGUFULI WAZAZI WAELIMISHWE

Kumekuwepo na sintofahamu nyingi kwa baadhi ya wazazi hapa nchini katika utekelezwaji wa agizo la mheshimiwa magufuli ikiwa ni moja kati ya ahadi zake wakati wa kampeni,mapema tu mwaka uliopita moja ya ahadi ambayo imeleta sintofahamu kwa baadhi ya wazazi hasa kwa kipindi hiki shule zinapokwenda kufunguliwa ni pamoja na ile ya elimu bure yaani pasipokuwa na malipo ya ada kwa shule za msingi na sekondari za serikali,suala hilo limeleta utata mkubwa kwa baadhi ya wazazi kwani wengine wamegoma kuwanunulia watoto wao hata mahitaji muhimu  kama sare za shule madaftari na kalamu,huku wakidhani kwamba suala hilo ni la serikali ya raisi magufuli
bado watanzania wengi wapo gizani kuhusiana na suala la elimu bure ,hivyo tunawaomba wadau pamoja na serikali kuwafikia wazazi wengi zaidi ili kuwaelimisha ni yepi majukumu ya wazazi na ni yepi majukumu ya serikali kuhusiana na sera ya elimu bure ili vijana wetu wapatiwe elimu iliyo bora.

0 Response to "ELIMU BURE YA MAGUFULI WAZAZI WAELIMISHWE"

Chapisha Maoni