ZA UKWELI SANA

TOYOTA YATENGENEZA GARI LINALOJIENDESHA.

Toyota imekuwa kampuni ya magari ya hivi karibuni kujaribu gari linalojiendesha bila dereva katika barabara ya uma.Gari hilo aina ya lexus Gs lilijaribiwa katika barabara ya tokyo shuto express ambapo lilionyesha ubora wake,ikiwemo kubadilisha laini za barabara na kukaa mbali na magari mengine.
Toyota imesema kuwa inalenga kuanzisha magari kama hayo ifikapo 2020,wakati ambapo mji wa tokyo utakuwa ukijiandaa kusimamia mashindano ya olimpiki.
 kulingana na toyota,gari hilo linatumia sensa kadhaa ili kubaini magari yaliyo karibu na kuchagua laini za barabara kwa lengo la kufika linakoelekea.matokeo hayo yanaonyesha kuwa gari linaendesha usukani,kichapuzi na breki sawa na vile binadamu wanavyoendesha magari yao.

0 Response to "TOYOTA YATENGENEZA GARI LINALOJIENDESHA."

Chapisha Maoni