ZA UKWELI SANA

WABONGO NA SIASA ZA USHABIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Watanzania walio wengi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25,wamepokea kwa namna tofauti hii inaonyesha ni kwa namna gani Demokrasia nchini Tanzania imekuwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na chaguzi nyingi zilizopita hili ni suala zuri sana.    

  Lakini kwa bahati mbaya sana wabongo baadhi yao wamekuja na mtazamo wa kishabiki kama ule tuliozowea kuuona kwenye simba na yanga,sasa huku jamani kwenye siasa mtazamo kama huo ni mbaya sana kwani watu wanashindwa kusikiliza sera za vyama vingine eti kwa sababu wanajiita wao ni chama fulani,hili sio zuri kwani hasara yake ni kukosa uamuzi sahihi katika kuchagua kiongozi sahihi na kukatisha ndoto iliyotarajiwa na wengi ya maendeleo,watu wanashindwa hata kusalimiana kisa utofauti wa vyama mahala pengine wanataka hata kupigana na kushindwa kusaidiana,kwasababu ya vyama.


   Ndugu zangu kumbukeni kuna maisha mengine baada ya Magufuli na Lowasa na pia baada ya uchaguzi sisi sote watanzania,tupendane tusigombane kama tunajenga nyumba moja tusigombee fito.
  
       NA MHARIRI WETU.

0 Response to "WABONGO NA SIASA ZA USHABIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU"

Chapisha Maoni