ZA UKWELI SANA

MCHANGO WA SANAA NA WASANII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015....

Wapendwa kukiwa bado na joto la uchaguzi mkuu napenda kuwakumbusha wasanii wote hasa wa muziki na bongo muvi wajameni nyinyi wasanii ni watu muhimu katika jamii zetu hapa nyumbani,na duniani kote kwa ujumla jamani hilo naombeni mlitambue,nyinyi mwaweza kupotosha jamii au kuikomboa jamii,kwa hivyo nadhani kwa kipindi hiki mngepashwa kuitumia sanaa yenu,kuwaelimisha wapenzi wenu umuhimu wa amani na kuchagua viongozi watakaolikomboa taifa.


  Lakini kinyume cha matarajio ya wengi mnawachanganya mashabiki wenu kwa kuangalia zaidi maslahi yenu hatukatai na nyie mnatafuta riziki lakini,mmejisahau mnatumika kama wapiga debe wa wanasiasa,wengine mkiwa huku wengine kule jamani MAMA TANZANIA KWANZA mengine baadae rudini kwenye mstari msaidie kutoa elimu kuhusu upigaji wa kura na mhamasishe amani nyinyi ni kioo cha taifa.

      NA Mhariri wetu jicho la kitaa Media.

0 Response to "MCHANGO WA SANAA NA WASANII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015...."

Chapisha Maoni