ZA UKWELI SANA

AFRICA NA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE

                    







   Africa ni bara lililobarikiwa sana na Mwenye enzi Mungu,licha ya changamoto kadha wa kadha zinazolikabili bara hili kama vile magonjwa,umaskini na ukosefu wa elimu ya kutosha na nzuri,bara hili limebaki kuwa masikini licha ya utajiri kibao uliopo katika bara hilo zipo sababu kadha wa kadha zinazo sababisha bara hilo kuendelea kuwa duni japo leo nitazungumzia baadhi ya mila kandamizi  zinazowakandamiza wanawake wa kiafrika,na siku nyingine nitazungumzia kwanini waafrika ni masikini licha ya utajiri mwingi waliokuwa nawo.

        kuna baadhi ya mila na desturi,ambazo bado zinashikiliwa na waafrika si nzuri na kinyume kabisa na haki za binadamu,lakini baadhi ya jamii za kiafrika zimeendelea kuzishikilia mila hizo,na bado hawataki kuziacha licha ya kupigwa vita vikali na jamii zilizoendelea,japokuwa kuna changamoto nyingi ikiwemo elimu ya kutosha kutowafikia jamii hizo;
      Baadhi ya mila na tamaduni hizo ni ukeketaji wa wanawake,au kuondoa sehemu ya siri inayo msisimua mwanamke inayofahamika kama kisimi au clitoris kwa lugha ya kigeni,eti kwa madai ya kumsafisha mwanamke na kumtoa tamaa ya ngono pindi mumewe anapo safiri na hivyo kutofanya mchepuko nje ya ndoa yake,lakini madhara ya kufanya tendo hilo ni mabaya sana tofauti na faida zake ambazo huwa chache za kimfumo dume na za kipuuzi,madhara yake ni makubwa husababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi mara anapofanyiwa tendo lile,na pia wakati wake wa kujifungua na mara nyingine hupelekea hata kufariki dunia,na mara nyingine husababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na kuchangia kifaa kimoja kwa watu wengi wakati wa kufanyiwa tendo hilo,na matatizo mengine mengi ya kisaikolojia.pia mwanamke wa kiafrika anakosa haki ya kumiliki mali kutokana na mfumo dume,haki ya kuwa kiongozi na haki ya kutokusikilizwa na kudharauliwa pia vipigo na unyanywasaji wa kijinsia katika ndoa.

      Huko nchini Lessoto kwa mfalme MUSWAT,kumekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa mabinti nchini humo ambao bado ni mabikira kutembezwa matiti wazi kama unavyoona pichani,na mfalme wa nchi hiyo kuchagua binti mmoja anayempenda na huu ni utamaduni uliodumu kwa miaka mingi,mabinti wanakatizwa masomo yao na kwenda kuolewa na ji baba hilo lenye uchu wa kimapenzi na lisiloridhika kamwe kwani mpaka sasa lina wanawake zaidi ya 40,watoto zaidi ya timu tatu za mpira,magari kibao huku wananchi wake wakiishi maisha ya ufukara kabisa.

waafrika lazima tuamke na tupige vita mila hizi kandamizi,hizi ni laana na tusipo badilika tutaendelea kuwa bara duni siku zote .



      




    usisite kututumia maoni yako
  kwa matangazo piga 0656538476.

0 Response to " AFRICA NA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE"

Chapisha Maoni