ZA UKWELI SANA

MWANAMUZIKI WA RAP WA MAREKANI AUWA.

Polisi nchini los angels inasema kuwa msanii wa muziki,wa rap kutoka marekani Marion suge knight  amekamatwa kutokana na mashtaka ya mauaji baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake na kumuua na baadaye kutoroka.

polisi wanasema kuwa bwana knight alijibizana na watu wawili katika eneo la kuegesha magari na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwengine akijeruhiwa vibaya.

wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.
suge knight ni mwanzilishi wa kampuni ya Death throw Records ambayo iliwazindua wasanii maarufu wa muziki wa rap kama snoop dog na marehemu Tupac shakur.

0 Response to "MWANAMUZIKI WA RAP WA MAREKANI AUWA."

Chapisha Maoni