ZA UKWELI SANA

HUU NI ZAIDI YA UKATILI.

Nilikuwa nikitafakari mahali wabongo tulipofikia,nadhani muda huu sasa ipo haja ya wabongo kumrejea mola wetu,maana matukio ambayo zamani yalikuwa ni adimu sana au nadra kutokea sasa ndio yanashamiri,gazeti hili la mtandao huu wa jicholakitaa linapinga vitendo vya ndugu zetu albino wanaouwawa na kuwindwa kama digidigi huku serikali ya Tanzania ikiwa imefumba macho na kuziba masikio kama hawaoni au hawasikii unyama huu,huku wanasiasa wakihusishwa zaidi na ukatili huu,kwani vimekuwa vikitokea nyakati za uchaguzi hilo halina uthibitisho lakini tunapatwa na mashaka kwani serikali inayoongozwa na kikwete kuonyesha imeshindwa kabisa,kullikabili hili kitu ambacho si kweli kabisa haiko tu sirias na haijaamua na haionyeshi kuamua.


kama serikali imefumba macho mimi na wewe msomaji tunajukumu la kuwalinda hawa ndugu zetu,kwani tunaishi nao miongoni mwa jamii yetu.Jamani hawa ni ndugu zetu tumetofautiana tu rangi za ngozi zetu na kila sehemu duniani wapo hata ulaya sio bongo tu,hivyo tubadilike huwezi pata utajiri kupitia viungo vyao,tuache hiyo ni aibu hawa ni watu kama sisi tena wanaweza kuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya mambo makubwa kwenye jamii hata zaidi yetu.


KAMA UNA HABARI AU TAARIFA WASILIANA NA MUHARIRI WA GAZETI HILI KWA NO;0656538476.
 

0 Response to "HUU NI ZAIDI YA UKATILI."

Chapisha Maoni