ZA UKWELI SANA

NEYMAR AWA TATIZO LIGI YA HISPANIA.

Kiungo mshambuliaji wa barcelona,neymar da silva jr,amekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu,ambapo amekuwa sehemu muhinu sana ya timu yake katika michezo ya hivi karibuni.

Neymar amedhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo amekuwa akifunga mabao mfululizo huku akisaidia kwa kutoa pasi za mwisho kwa wenzie na amekuwa akifanya hivyo kwa mwendelezo mzuri.

Tatizo limekuwa moja tu,jinsi ambavyo mchezaji huyo amekuwa akilaumiwa hasa na wapinzani kwa kuwa mtovu wa nidhamu na mkosefu wa heshima ambapo amekuwa akiwadhihaki wachezaji wa timu pinzani kwa nyakati tofauti hali ambayo imeonekana kuwakera wengi.
 
Neymar amekuwa na tabia ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani,na ndio maana amekuwa kwenye vurugu nyingi ambazo zimekuwa zikitokea kwenye michezo ya fc barcelona.

majuzi wakati wa mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la mfalme ambapo barcelona ilishinda kwa 3 kwa 2 neymar alikuwa kwenye fujo zilizoibuka kati yake na wachezaji wa atletico ambao ni Gabi,juan fran na raul garcia.

ilifikia mpaka kocha luis enrique alilazimika kumtoa uwanjani,ambapo baadae alikiri kufanya hivyo kwa lengo la kumlinda.

hivi karibuni luis enrique alisikika akisema kuwa neymar anapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wapinzani na kama asipofanya hivyo huenda akafanywa chambo na kuumizwa na wachezaji wa timu pinzani ambao wamejawa na hasira juu yake.

tabia hii ya neymar itawakumbusha wengi juu ya kile,kilichokuwa kinafanywa na Ronaldinho Gaucho wakati akiwa na klabu hii ya barcelona ambapo aliripotiwa kuwadhihaki wapinzani huku akiendelea kuwakera kwa chenga zake za maudhi.

0 Response to "NEYMAR AWA TATIZO LIGI YA HISPANIA."

Chapisha Maoni