ZA UKWELI SANA

Taarifa mpya Kuhusu lile gari la Ikulu Lililoibwa Kenya.

  jumatano ya wiki iliyopita ndio liliibwa hili gari aina BMW lisilopenya risasi ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa raisi Kenyata,na taarifa ya ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake ambae ni askari alikua akielekea kwenye makazi ya polisi Nairobi,njiani akasimamishwa na watu waliokuwa na Ak 47 wakamtupa mtaroni baada ya kumvua nguo na kukimbia nalo.
   Taarifa mpya inaripotiwa na ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich inasema gari hili limepatikana kwenye mji wa Tororo Uganda na Tayari limepelekwa Kampala baada ya msako uliofanywa na polisi na kumkamata mmoja hotelini mjini Bungoma.

   Kikosi cha Flying Squard kikishirikiana na Interpol walivuka boda na kuingia mji wa Tororo Uganda,walikohisi kwamba ndiko kuliko pelekwa gari hilo.

Gari liloibwa.

0 Response to "Taarifa mpya Kuhusu lile gari la Ikulu Lililoibwa Kenya."

Chapisha Maoni