ZA UKWELI SANA

Jumba la BBA lateketea Kwa moto.

  Jumba lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya washiriki wa shindano la Big Brother Africa(BBA)2014 limeteketea kwa moto jana eneo la Sesani Studies jijini Johannersburg nchini Afrika kusini.
 

Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kufanyika jumapili ijayo ya Septemba 7,mwaka huu.
   Kwa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa shindano hilo la M-net na Endemol ni kwamba katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na chanzo cha moto huo hakija fahamika huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo chake.

0 Response to "Jumba la BBA lateketea Kwa moto."

Chapisha Maoni