ZA UKWELI SANA

NYANI AGAWA PESA INDIA.

walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa nyani huyo kwa jina Simian aliiba fedha kiasi cha rupee 10,000 kutoka nyumba ya jirani katika eneo hilo. Nyani huyo aliingia katika nyumba hiyo kutafuta chakula lakini alipokosa akaamua kutoweka na pesa. jimbo la Himachal pradesh imekuwa makao kwa wanyama wengi ambapo kuna takribani nyani 300,000,nyani aina ya macaque,huonekana kama wanyama wa kuabudiwa na hivyo hulishwa na wananchi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanyama hao,wamekuwa wakizozana na wakazi kwa sababu ya kuharibu mimea kushambulia watu na hata kuwauma watoto . Maofisa tayari wametangaza wanyama hao kuwa kero kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo. Nyani huyo mwanzo alionekana akiwa ameketi juu ya paa la nyumba akiwa na bunda la noti kabla ya kuanza kuwagawia watu pesa hizo kwa kuwarushia. Watu walipoanza kukusanya pesa hizo,nyani huyo alikimbilia kwenye mti mwingine,watu waliendelea kumfuata"alisema mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo. HABARI NA BBC.

0 Response to "NYANI AGAWA PESA INDIA."

Chapisha Maoni