ZA UKWELI SANA

EBOLA DAMU YA WALIOPONA KUTIBU UGONJWA.

shirika la Afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wamepona ugonjwa wa ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine. Katika mkutano mjini Geneva,wataalamu wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,Sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo. Wataalamu hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zingine mbili. Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili. Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana. CHANZO BBC.

0 Response to "EBOLA DAMU YA WALIOPONA KUTIBU UGONJWA."

Chapisha Maoni