ZA UKWELI SANA

Maneno Mengi na Madeni Mengi Havitusaidii Sana.

  Hakuna haja ya kuandika maneno mengi zaidi,kuthibitisha kile kijielezacho chenyewe waziwazi.Ukweli huu juu ya mikopo na madeni ni wa wazi unaosimama imara katika kujieleza wenyewe kuwa idadi kubwa ya madeni haimfanyi mtu awe tajiri bali huweza kumfanya awe masikini zaidi.
   Hata nchi zenye madeni makubwa huwa katika orodha ya nchi masikini wakati wana uchumi wanapokokotoa uwiano wa rasilimali za kimtaji na akiba ya fedha za kigeni zinazomilikiwa na nchi hizo dhidi ya kiasi cha madeni zinavyodaiwa.
   Inawezekana kuishi na kuendesha maisha yako ukiwa kulia kwa sifuri na si kuendesha maisha ukiwa kushoto kwa sifuri.Ni hatari kuwa kushoto kwa sifuri katika dunia hii isiyo na huruma kwa wadaiwa.

Je madeni ni Mbinu Madhubuti ya Mafanikio?:-

Unaweza kujibu swali hili litokalo mwanzoni mwa sura hii.je madenj ni mbinu madhubuti ya mafanikio?pia,muulize mwenzi au ndugu yako au rafiki yako mjadili majibu yenu.

  Ikiwa Mungu atakusaidia ukalipa madeni yote unayodaiwa je,utapenda kukopa tena na kurejea kwenye madeni?kwa nini kufanya hivyo ni hatari kwa mafanikio yako maishani

0 Response to "Maneno Mengi na Madeni Mengi Havitusaidii Sana."

Chapisha Maoni