ZA UKWELI SANA

CCM,CHADEMA WAWA GOMBANIA BODA BODA IRINGA MJINI.

  Mbunge wa jimbo la Iringa mjinj,mchungajj Peter Msigwa(chadema)ameahidi kuchangia sh Milioni tatu na pikipiki (boda boda) kumi kwa chama kipya cha boda boda kinachotarajiwa kuanzishwa kwa utaratibu wa ofisi yake wakati wowote kuanzia sasa .
   Hilo likitimia kutakuwa na vyama viwili katika manispaa ya Iringa vya madereva boda boda vyenye Itikadi tofauti za kisiasa,ambapo hivi sasa kuna chama cha madereva boda boda na bajaji ambacho kinadaiwa kuwa na wanachama wengi wa CCM ambacho mwenyekiti wake ni ndugu joseph.
    kumekuwa na manung' uniko kwa wadau hao wa boda boda mjini Iringa kwamba chama kwa sasa hakiwajali na kinajali maslahi yake na hivyo wamemwomba mbunge huyo wa kuwasaidia kuanzisha chama kipya ambapo alipohojiwa ndugu joseph mwenyekiti wa boda boda amesema mbunge huyo anataka kuwagawa tu kwani alimwambia atamuhitaji kwenye mkutano na badala yake aliitisha mkutano bila kumtaarifu,wakati mbunge akiitisha mkutano na yeye ndugu joseph alikuwa kwenye mkutano na wanachama wake.

Mbunge Msigwa amesema atawasaidia madereva hao wa boda boda lakini si kwa lengo la kupata kura mwakani,wakiona anafaa wamchague kama hafai wasimchague,na suala kujiingiza kwenye vyama vya pikipiki si la lazima unaweza kuingia upande unaopenda na unaweza kujitoa vile vile.

Kuhusu Malalamiko kwa mwenyekiti wa chama hicho cha boda boda ndugu Joseph ameeleza kwamba madereva wanao lalamika wengine si wanachama wa chama hicho bali wanashirikiana tu kama madereva wenzao lakini hawashirikishwi kwenye mambo ya chama hivyo wanalalamika kwa mambo wasio yajua alidai chama chake kinawachama 171 tu na katika manispaa ya Iringa kuna wanachama zaidi ya 1000.

0 Response to "CCM,CHADEMA WAWA GOMBANIA BODA BODA IRINGA MJINI."

Chapisha Maoni