ZA UKWELI SANA

TUMIA FIKRA NA MAWAZO YAKO VIZURI UPATE MANUFAAA

Vitabu vya dini vya miaka mingi haswa biblia vilishaandika kwamba 'afikiriavyo mtu ndivyo alivyo'unafikiria nini juu ya maisha yako kushinda au kushindwa?wacha mawazo duni au kujikataa mwenyewe kabla hujakataliwa na watu kuna watu wale wale ambao ni chronic worriers,waoga chronic ambao wao hawawazi mambo ya kufurahisha mioyo yao huwaza mawazo ya uharibifu tu kama kufilisika,kupata ajali,kufariki au kusimamishwa kazi,hiyo ni hatari sana kwa ustawi wa maendeleo yako,kwani ukiendelea kuweka fikra na mawazo ya uharibifu akilini mwako,baadae hujakudhihirika katika maisha halisi ndio maana tunashauriwa kufikiria na kuwaza fikra na mawazo yenye mbolea tu maishani mwetu
mambo  mabaya maishani mwetu yapo na hatuwezi kuyaepuka kwa sababu kila jambo hapa duniani hutokea kwa mipango ya mungu,lakini hatupaswi kuzama katika mawazo hayo wala kuhofia sana,kwani kuendelea kuwaza ni kujipatia maumivu zaidi na zaidi kabla ya matatizo yenyewe kutokea,na pia jinsi unavyozama kwenye mawazo mabaya unakaribisha hatari kuwa karibu yako zaidi,acha kufikiria maisha ni uchaguzi umepewa nafasi ya kuchagua kwa kutumia mawazo yako kuwa na furaha au huzuni mungu anafanya kazi kupitia mawazo yako waza positive na sio negative hatma yako ipo kwenye mawazo yako.
 

0 Response to "TUMIA FIKRA NA MAWAZO YAKO VIZURI UPATE MANUFAAA"

Chapisha Maoni