ZA UKWELI SANA

TENGENEZA MAISHA YAKO KUWA YA FURAHA ZAIDI

By yusuph mbuguni
               ndugu msomaji habari za siku kama hii ya leo,bila shaka upo salama na afya tele basi kwa wale wagonjwa mwenyezi mungu na akawaponye,najua mpendwa dunia hii ya leo yenye pilika,pilika za kimaisha stress ni nyingi sana haswa ukizingatia zote zinaletwa na hali ngumu za kiuchumi,pesa imekuwa ngumu kupatikana hivyo watu wengi hushindwa kujitimizia mahitaji yao muhimu au ya familia zao,hivyo watu hushindwa kutambua ni mbinu gani sahihi za kuweza kutatua matatizo yao,wengine huchanganyikiwa hufikia hatua za kuongea wenyewe mabarabarani,wengine hushindwa kujikontroo na kuamua kuukatisha uhai wao kwa namna yeyote ile;lakini haya yote yanatokana na kutokuujua ukweli juu ya maisha na imani juu ya mwenyezi mungu kutatua changamoto za maisha yetu wanadamu,watu wengi wanasema wanamuamini mungu,lakini sio kweli watu wengi wanaogopa wakisikia habari za mungu lakini hawana imani naye pindi wapatapo matatizo,utamkuta mtu apatapo shida kidogo huanza kulalamika wengine kufikia hatua ya kusema maneno ya kufuru kabisa na wengine hufikia hatua ya kumtangazia kila mtu shida zake,iko wapi imani yake tena?nimekuja kubaini katika uchunguzi wangu kwamba watu wengi hawana elimu ya 'reality of nature'yaani uhalisia wa maisha na 'law of nature'sheria ya ulimwengu ambayo jaji wake ni mwenyezi mungu,watu wengi wapatapo shida kidogo huanza kuhaha wao wanayaita ni matatizo hapana sio vyema kuyaita matatizo kwa sababu matatizo ndani yake kuna maumivu na hakuna makusudio mazuri,ningependa uite ni changamoto za kimaisha tu,kwani kwenye kila msukosuko unaopitia basi sheria ya mungu inasababu ya kukupitisha hapo ulipo,ni vyema ukaiweka hii katika akili yako ya kwamba kila jambo linalotokea juu ya maisha yako ni mungu pekee ndiye hupanga,na changamoto zozote unazopitia maishani hazina malengo ya kukuumiza kama unavyodhani bali zina malengo ya kukupa funzo ni namna gani uishi au uenende katika maisha yako hakuna kitu ambacho hutokea kwa ajali au kwa bahati mbaya kila kitu hupangwa na hiyo ndiyo huitwa 'law of nature'jambo liwe baya au zuri yote yamepangwa na mwenyezi mungu,unachopaswa kufanya ni kumuamini mwenyezi mungu sana na kumshukuru kwa kila jambo pia weka katika akili zako ya kwamba hakuna changamoto ya kudumu maishani zote ni temporaly tu zote ni kwa wakati fulani tu kisha baada ya kukupa funzo alilolipanga mwenyezi mungu hupita na kukuacha salama salmini,acha kutengeneza mawazo potofu kama,mimi nina mkosi au nuksi,nina laana au nimerogwa hapana ukileta mawazo na fikra kama hizo mbaya ndio unazidisha matatizo zaidi na inakuwa si changamoto tena,siku zote muamini mwenyezi mungu na umpe nafasi maishani mwako,na fikiria mawazo chanya au mazuri tu maishani mwako,fikiria upendo palipo na chuki,fikiria amani penye vita,fikiria pia kupata kwenye kukosa,fikiria utajiri penye umasikini,fikiria shibe kwenye njaa,nakadhalika na kadhalika mwanadamu ukiweza kuinkontroo akili yako basi utaishi kwa amani,hakuna jambo lolote la nje linaweza kukuumiza bila ya kushirikisha fikra zako hasi au mbaya fikiria kuwa na furaha maishani mwako acha kuifanya dunia yako kuwa chungu wewe mwenyewe.
 0656538476

0 Response to "TENGENEZA MAISHA YAKO KUWA YA FURAHA ZAIDI"

Chapisha Maoni