ZA UKWELI SANA

TAFAKARI NA KUMBUKUMBU KIFO CHA NYERERE

Tarehe 14 octoba kila mwaka hapa nchini Tanzania,tunaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere,leo ikiwa ameshatimiza miaka takribani 16 tangu atutoke,tujitafakuri wabongo tunamuenzi vipi mwalimu nyerere haswa kwa yale mema aliyotuachia,imekuwa ni kawaida watu maarufu au viongozi wa kiserikali kutumia maneno na misemo yake ya kifalsafa lakini ni ngumu katika Tanzania ya leo kukuta,maneno yake hayo yakitumiwa na viongozi wa taifa hili kwa vitendo,ubinafsi matabaka baina ya walio nacho na wasio nacho yameongezeka,udini na ukabila ndio usiseme,tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu oktoba 25,napenda kuwa kumbusha wabongo wenzangu tukumbuke misingi aliyotuwekea mwalimu nyerere hapo tutakuwa tumeacha unafiki na kumuenzi mwalimu kwa dhati kabisa.

0 Response to "TAFAKARI NA KUMBUKUMBU KIFO CHA NYERERE"

Chapisha Maoni