ZA UKWELI SANA

MAKAMANDA WA CHADEMA WAFANYA KUFURU MUHEZA.

Wakati joto la uchaguzi likizidi kuendelea kuwa kali hapa nchini na wagombea wakizidi kuuza sera zao,huko mkoani TANGA wilaya ya muheza siku ya jana walifurika wakazi wa muheza katika viwanja vya majani mapana kusikiliza sera za mgombea ubunge kupitia chama cha chadema chini ya mwamvuli wa ukawa ndugu kamanda Ernest Msingwa,katika hali isiyozoeleka kwa wakazi wengi wa Tanga na haswa wilaya ya muheza,mara hii chadema imeonekana kupendwa sana na kujaa kwenye kampeni zao kila mikutano inapoitishwa,huku mgombea wa tiketi ya ccm ndugu Balozi Adadi rajabu akiambulia watu wachache baadhi ya wazee na akina mama wachache ambao ni makada wa chama hicho,hali inayoonyesha kufa kisiasa kwa ccm wilayani humo na kuchokwa na watu kwa ahadi zao butu kwa wananchi,baada ya msingwa kumaliza kampeni jana jioni baada ya kushushwa na askari polisi aliwaambia polisi wakumbuke kutenda haki kwa vyama vyote,ndipo wananchi walipo mwomba mgombea huyo kuingia katika gari lake na wamsukume huku wakiimba nyimbo kama 'huyo adadii....hatumtaki..hatumtaki..' hali inayoonyesha wazi mgombea wa ccm kupitia chama hicho kupingwa na wakazi wengi wilayani humo.
 pichani kamanda ERNEST MSINGWA MGOMBEA wa ubunge wa chadema kupitia mwamvuli wa ukawa kwa jimbo la muheza.

0 Response to "MAKAMANDA WA CHADEMA WAFANYA KUFURU MUHEZA."

Chapisha Maoni