ZA UKWELI SANA

KUTANA NA MCHEKESHAJI MC PILIPILI,MWENYE MAFANIKIO

Nadhani jina la mc pilipili litakuwa sio geni masikioni mwako,au hata umeshawahi kumuona kijana huyu mchekeshaji kupitia kazi zake,mc pilipili ni kijana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita huko kijijini kwao dodoma,mc pilipili alianza kazi ya uchekeshaji tangu shule ya msingi,na baadae alisomea ualimu wa sekondari na kufanya kazi ya kufundisha kwa miaka 6,na kuamua kuacha kazi na kwenda DAR,ambapo huko alijifunza stand up comedy na kuanza kutumia mbinu ya kuchekesha na kuwa mc kwenye maharusi mbalimbali,ambapo aliweza kupata umaarufu kwa haraka sana,na kuweza kuajiriwa kama mtangazaji mchekeshaji na kituo cha radio cha times fm na kipindi cha the clip tv1,mc pilipili ameweza kujipatia umaarufu mkubwa kupitia sanaa yake ya uchekeshaji majukwaani na pia kipato kimeongezeka amefungua ofisi yake maeneo ya sinza amenunua gari ya fahari amejenga nyumba nzuri na anamiliki viwanja pia,mc pilipili aliweka uwoga pembeni alithubutu na akaweza pia hata wewe ukithubutu ukiwa na nia utaweza kufanikiwa kwenye utafutaji wako pia,hongera mc pilipili kwa kutimiza miaka thelatini na leo ni siku yako ya kuzaliwa happy bellated day kaka.
kila la heri mc washawasha.

0 Response to "KUTANA NA MCHEKESHAJI MC PILIPILI,MWENYE MAFANIKIO"

Chapisha Maoni