ZA UKWELI SANA

RAYC ARUDISHA KIUNO BILA MFUPA.

Msanii mkongwe wa muziki hapa nchini Rehema chalamile almaarufu kama Rayc  ameonyesha furaha yake kupitia mtandao wa instagram baada ya kuandika kwamba anashukuru mwili wake ule wa zamani wa umiss uliokuwa ukimtambulisha kama kiuno bila mfupa kuwa umerejea na kwamba mameneja wamuziki hapa nchini kama akina babutale na fella wajiandae kufanya naye kazi,Rayc aliripotiwa kutumia madawa ya kulevya miaka kadhaa nyuma iliyopita mpaka pale muheshimiwa raisi kikwete alipoamua kumnusuru kwa kumpeleka kwenye kitengo cha waathirika wa madawa ya kulevya na kuanza kupatiwa tiba ya dawa aina ya methadone na ndipo hapo rayc alipojiachia mwili na kuwa kibonge baada ya kupatiwa dawa na matibabu,hali iliyomkera rayc kurudi kwenye sanaa kwa kupoteza muonekano wake wa awali,rayc aliamua kufanya mazoezi na aliripoti kupitia mtandao wake wa instagrram kwamba amepungua kwa zaidi ya kilo 30,
hizi baadhi tu ya picha zikionesha muonekano mpya wa rayc kwa sasa.

0 Response to "RAYC ARUDISHA KIUNO BILA MFUPA."

Chapisha Maoni