ZA UKWELI SANA

NI MUDA WAKO WA KUAMKA SASA KIJANA.

MAKAZI YA MALOFA.
Kijana ukichagua vibaya,utampata kiongozi mbaya,mwaka huu ni mwaka wa kufanya maamuzi,sahihi Tanzania ina rasimali nyingi sana,lakini watu wake wanaishi maisha magumu sana,watoto wa masikini ambao wanaitwa malofa wanasoma katika mazingira magumu sana,na wengine hawasomi kabisa,na wanaobahatika kusoma hawapati elimu bora matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho yanaongezeka siku hadi siku,matajiri wanazidi kutajirika zaidi na masikini wanazidi kuwa masikini zaidi hili sio sawa kabisa,ni lazima vijana tukubali kuibadilisha hii hali,nimewalenga vijana zaidi kwa sababu vijana ni wengi zaidi kuliko wazee,tusikubali kudanganyika na ahadi kibao za kampeni ambazo hazitekelezeki,na hata kama  zinatekelezeka wanashindwa namna ya kutekeleza kwa sababu zao za ubinafsi,sikwambii mchague nani wala chama gani kwa sababu kila mtu ana maono na nchi yake,na anajua ni kiongozi gani anayeweza kulifikisha taifa hili mahala pazuri zaidi,tuache ushabiki wa kisiasa siasa si mchezo wa mpira,tusikilize sera za viongozi wote,na vyama vyote kisha ndio tuweze kuwapima,nasikitishwa na ushabiki unaoendelea kwani sio wa kujenga kabisa.
         Tanzania ni moja tuilinde amani ya nchi yetu,tukapige kura kuchagua viongozi bora,watakaotuongoza vyema.
 mungu ibariki sana TANZANIA
  piga 0656538476 ..

0 Response to "NI MUDA WAKO WA KUAMKA SASA KIJANA."

Chapisha Maoni