ZA UKWELI SANA

NANI KWAKO NI MWAUME AU MWANAMKE JASIRI?

          
Kwako wewe unamtamfisiri vipi mwanaume jasiri au mwanamke jasiri?je ni yule aliyejazia kifua na kuwa na misuli mingi?ni yule mwenye hasira nyingi au kuwa na nguvu nyingi?bila shaka kila mtu anatafsiri kivyake dhana hii na anaweza kuwa na majibu sawa na haya au tofauti kabisa na haya lakini wengi wetu tuna tafsiri ambayo sio sahihi sana ya strong man au strong womam,Tasiri ambayo inaweza kuwa sahihi ya mwanaume jasiri au mwanamke jasiri ni yule mtu ambaye ana misuli ya kukabiliana na nyakati ngumu mbalimbali ambazo anazipitia,kwa mfano kupunguzwa au kufukuzwa kazi,kuachwa na mpenzi,au mume au mke,na matatizo mengi mengi ambayo yatamtikisa kidogo,ambaye hayupo tayari kukata tamaa,wala kujutia anayoyapitia,kuna watu wanafikia hatua ya kujiua kwa sababu ya kufeli tu mitihani je umeshawahi kujiuliza kuna watu ambao hawasoma kabisa na wana maisha mazuri?
Wapo wanaolalama wanakula ugali na dagaa kila siku,je umeshajiuliza kuna watu kuupata hata huo ugali ni  shughuli  pevu?? au wapo wanaolalia mlo mmoja tu kwa siku?hiyo ni roho ya kinyonge na dhaifu na isiyo mshukuru mungu,yakupasa ufahamu no permanent situation in life,hakuna hali ya kudumu unayopitia katika maisha yote ni mapito tu na ipo siku yatapita,jua kusudi la mungu juu ya maisha yako hata katika vitabu vya dini tunamsoma nabii yusuph ambaye aliuzwa misri na nduguze akapitia mapito mengi na kufikia hatua ya kufungwa gerezani lakini mwisho wake ulikuja kuwa mzuri na kuwa waziri mkuu wa misri,je akijinyonga angefikia pale?yatupasa tu fahamu hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kila kitu kinatokea kwa mipango ya mungu,wala sio kwamba Mungu ametutupa hapana,tunapitia hayo ili kutupa somo katika maisha na kutufanya tumkumbuke kwamba mungu yupo.
    a strong man is he who stand alone,simama mwenyewe  usitegemee akili zako mwenyewe,mtegemee mungu kwa kila jambo jua  kusudi la mungu juu ya maisha yako,wacha kulilia baba,wacha kulialia mama,wacha kubabaika kijana kuna watu wana magumu kuliko yako bado wanafurahi na kumshukuru mwenyezi mungu.

          piga 0656538476 kwa matangazo ya biashara.

0 Response to "NANI KWAKO NI MWAUME AU MWANAMKE JASIRI?"

Chapisha Maoni