ZA UKWELI SANA

NAMNA YA KUFIKIRI NA KUPATA MAFANIKIO.

Mungu mara zote amekuwa akifanikiwa katika mipango yake,mwanadamu naye anapaswa kufanikiwa kwa sababu mungu yupo ndani yake,mipango,ubora na uweza wa mungu upo ndani yake mwanadamu.Mwanadamu ameumbwa ili kupambana akili,maarifa na nguvu zipo pamoja na yeye,zinasubiri kutolewa na kumfanya ashinde magumu yote,kuna watu wengi wanatumia dhana yamafanikio,mara kadhaa mpaka wanayapata mafanikio yao,kumbuka mawazo yote ya mafanikio yanakusanya chembechembe za mafanikio,kama mtu anarudia neno mafanikio katika fikra zake kwa imani na shauku,nafsi yake itaamini kweli anataka mafanikio,na kweli  kwa uweza wa mungu atakwenda kufanikiwa.Jambo kubwa mtu analotakiwa kujua ni kitu gani anachotaka kufanikiwa,kama mtu hufahamu ni kitu gani unachotaka inaweza ikawa sio rahisi kufanikiwa ni lazima kila mtu aishi na nia na malengo thabiti,kama hujui cha kufanya ni vyema kumshirikisha mungu sana kwani kwake upo ushindi.
mtu lazima uamini una nguvu ya kutengeneza  jambo ndani yako,iache hiyo nguvu iwe na shauku chanya,nguvu hiyo ambayo mwanadamu upo nayo ni ya kutengeneza jambo kwa kutumia fikra zako,kujua hiyo nguvu uliyonayo ndani yako na kutumia kanuni kutasababisha uoga,mashaka,hofu kupotea kabisa.

    Kama mtu atajiingiza katika fikra za kushindwa,fikra hizo hizo za kushindwa zitamvutia yeye kushindwa  nafsi yake itachukulia fikra za kushindwa kama maombi yake na zitaendelea kudhihirika kwenye shughuli zake binafsi,kwa sababu amefikiria kushindwa na fikra hazijui kuchagua jambo la kufikiri,mpaka uzikontrol wewe mwenyewe.Mfanya biashara mmoja rafiki yangu ambaye ni fundi wa kushona nguo,anapenda kutumia msemo msemo huu ''ninachofanya siku zote nikuongeza''Alimaanisha kwamba mafanikio ni ishara yakuongeza,kuongeza utajiri wako,nguvu,imani,na maarifa.Maisha ni kuongeza,kifo ni kupunguza na utaweza kuongeza mafanikio yako katika maisha kwa kufikiria vitu vya ukweli,upendo na vya kuleta matumaini,fikiria na pia tengeneza hisia za kufanikiwa na lazima utafanikiwa,wewe sio mtumwa wa matatizo,mazingira au hali zozote zile kwenye maisha,wewe ni mkuu wa hali zote,unaweza kuwa mwathirika wa hali kwa fikra zako namna unavyofikiri mambo.Ukibadilisha fikra zako na utakuwa umebadilisha hali yako pia ya kimaisha,tengeneza fikra ya vitu unavyopendelea kuvifanya au unavyopenda kuvipata,fikiri kwa akili zako na ushiriki kiuhalisia wa kufanikiwa.Jenga tabia hiyo mara kwa mara,nenda kitandani ukiwa una fikiria kuhusu mafanikio yako kila usiku,utafanikiwa kwa kupandikiza mawazo ya mafanikio katika fikra zako,kumbuka wewe ni kile unachofikiri na afikiriavyo mtu ndivyo alivyo,fanya kazi kwa bidii na umtegemee mungu na kutumia kanuni hizi utafanikiwa.


   

tumia namba hii kwa matumizi ya ofisi tu 0656538476

0 Response to "NAMNA YA KUFIKIRI NA KUPATA MAFANIKIO."

Chapisha Maoni