ZA UKWELI SANA

MAISHA NI MCHAKATO

Ndugu zangu wapendwa,habari za jumatatu hii ya leo,wengi hupenda kuuita blue Monday,kutokana na uchovu na pilika na pilika za kutoka out,na wengine baadhi yao hunogewa na mapumziko haya ya siku mbili walioyatumia kukaa na familia zao,wapenzi wao ndugu jamaa na marafiki,hivyo wanaona tabu,kuanza siku mpya tena,wakiwa kazini,pamoja na hayo yote ndugu zanguni lakini tukumbuke maisha lazima yaendelee na ili yaendelee na ili yaweze kuendelea vizuri ni lazima tufanye kazi,tena kufanya kazi kwa bidii bila kubweteka.

Hivi ikaribuni kumekuwa na wimbi kubwa la vijana hasa wanaotamani kuwa na maisha mazuri,labda kama fulani au kama fulani,si jambo baya kuwa na uchu wa maisha  maisha bora,ni jambo zuri tu,lakini ambacho hawakifahamu ni namna gani au mbinu gani haswa zimetumiwa na hao watu kupata hayo maisha ambayo leo vijana wengi wanayatamani.
SAID SALIM BAKHRESSA.
Jambo linalowafanya vijana wengi kujiingiza katika vitendo hatarishi ambavyo wanaamini kupitia vitendo hivyo huwenda wakafanikiwa kwa haraka zaidi,jambo ambalo si la kweli,na wala sio ukweli halisi wa maisha na pia sio sheria ya mwenyezi Mungu,ukweli halisi ni kwamba maisha ni mchakato,kuna mwanamuziki mmoja wa injili hapa nchini aliwahi kusema maisha ni foleni,hili ni kweli kabisa,maisha yanahitaji kujituma sana bila kuchoka,kuwa mtu asiyekata tamaa,pia kutokubali kukatishwa tamaa kwa ndoto zako za mafanikio unazoziota kila siku.
diamondplatnuzm
fahamu mtafutaji mwenzangu adui yako mkubwa katika harakati zako ni kukata tamaa na kuogopa kujaribu unachoona kinaweza kukusogeza katika harakati zako za utafutaji,kumbuka wakati wewe unapokata tamaa kuna msemo waswahili hupenda kuutumia ya kwamba baada ya dhiki ni faraja,na unapoona matatizo yanaongezeka sana jua ushindi umekaribia kwa maana ufunguo wa neema upo chini ya moto,au umesahau riziki ni mafungu saba?huna haja ya kuacha kuzisogelea ndoto zako,huenda fungu lako ni la sita,sasa foleni ipo fungu la tano zamu yako itafika tu usiogope,huna haja ya kufanya shortcut maisha yanahitaji uvumilivu.
MENGI
haijalishi umehangaika mara kadhaa,kutafuta kutoboa kimaisha,lakini unashindwa,endelea kujifunza zaidi kwa watu waliofanikiwa soma vitabu hasa vya ujasiriamali na vyenye mafunzo ya kimaisha,tumia vyema kipaji chako alichokupa mungu bila kuogopa wanadamu wala kuona aibu,hata hao waliofanikiwa walijaribu mara nyingi bila kuona aibu,bila kukata tamaa,usiogope kudharauliwa na hata kukatishwa tamaa,si kiliza mtu wako wa ndani ambaye ni nafsi yako inataka nini?ndipo sa unaweza kufanikiwa,mwisho kabisa mtegemee mungu wako kwa kila jambo.

PIGA 0656538476 KWA BIASHARA TU.

0 Response to "MAISHA NI MCHAKATO"

Chapisha Maoni