ZA UKWELI SANA

HILI NDIO FUNZO ALILOLIACHA DJ FETTY KWA WATU.

Add captionDJ FETTY.
siku ya jana septemba 16,mwaka 2015 haita kaa isahaulike kwa wafanyakazi wa clouds fm radio,na clouds media kwa ujumla,na hata wapenzi wa clouds fm radio na wasikilizaji wa kipindi cha mchana cha xxl,pamoja na so,so fresh cha jumamosi usiku,hii ni mara  baada ya mmoja wa madj na mtangazaji wa muda mrefu wa radio hiyo dj fetty,kuamua kuacha kazi rasmi,na kwenda kuendeleza biashara zake binafsi,jana mchana aliwaaga rasmi wafanyakazi wenzake,na wasikilizaji wa radio hiyo pendwa ya vijana,hafla hiyo ilihudhuriwa na watangazaji wenzake wa muda mrefu,bdozen na adam mchovu,watangazaji wengine na baadhi ya wasanii kama godzla ambaye alielezea kwa urefu tangu amfahamu fetty na kudai kamwe hataacha kumshukuru kwa sababu yeye ndiye aliyemtoa,wengine waliemuelezea fetty ni pamoja na johmakini na gnako,wengine hawakuwepo studio lakini waliweza kutuma ujumbe wa sauti ukasikika hewani ambao ni benpol,mwasiti almasi na diamond platnumz ambao wote walimshukuru kwa kuwasaidia na kumtakia  maisha mema katika kazi zake nyingine,fetty alielezea jinsi alivyofanya kazi vizuri na adam mchovu na bdozen 

    kiukweli tuliishi kama family japo tulikuwa tunagombana lakini yanaisha,alisema fetty,ni wakati mgumu kwangu na kwa wote llakini inabidi maisha mengine yaendelee alisema fetty kwa huzuni sana.

funzo tunalopata hapa ni kwamba tukipata fursa ya kufanya kazi tufanye kwa bidii kama ilivyokuwa kwa fetty alithubutu na kuwa inspaya vijana wengi wa kike kuwa madj na watangazaji pia,kwani yeye ndiye alikuwa dj wa kwanza mwanamke,na ndiye dj pekee kutoka afrika mashariki kuitwa kupafomu big brother,na pia fetty ametufundisha kwamba mafanikio siyo kuwa na mali nyingi bali ni kusaidia watu kutimiza ndoto zao,na kutoa msaada kwa wasio na uwezo kama alivyofanya fetty,kuna wakati msanii ruby anasema alikwama kifedha fetty alimsaidia laki mbili,kitu ambacho kutoa hasa pesa ni vigumu kwa wakati huu,kila aliyemzungumzia fetty alimzungumzia Kwa mema,wafanyakazi wenzake walimsihi sana asiondoke,wasanii na hata wasikilizaji walisikitika sana kuonyesha mapenzi yao kwa fetty.
dj fetty ni mfano wa kuigwa na wengi tuwekeze katika watu hata tukifa leo tukumbukwe kwa mema tuliyoyaacha Sio kuwa na mali nyingi,fetty alikuwa ni mtu wa wawatu,funzo jingine ni kwamba tukipata ajira au vibarua tusijisahau tukumbuke na kuwekeza pia,fetty ameamua kuacha kazi na kufanya kazi zake mwenyewe kwenye kampuni yake inayoitwa fettylicious company,na duka lake la nguo liliopo dar free market. 

0 Response to "HILI NDIO FUNZO ALILOLIACHA DJ FETTY KWA WATU."

Chapisha Maoni