ZA UKWELI SANA

FIKIA MAFANIKIO YAKO SASA.W

Watu wengi wamekuwa wakizungumzia sana mafanikio,na wengi tunatamani kufanikiwa kwa namna yeyote hapa duniani,lakini kila mtu anatafsiri yake binafsi kuhusiana na hili neno mafanikio,inanisikitisha sana kila mara ninapokuwa nazungumza na watu mara kadhaa ninapokutana nao,wananiuliza maswali kama,aina gani ya nyumba unayoishi,magari mangapi unayoyamiliki,je una bwawa la kuogelea nyumbani kwako??haya masuali yananifanya nifikiri kwamba watu wengi hawana tafsiri sahihi ya neno kufanikiwa,japo mtu aiyefanikiwa pia anaweza kumiliki mali hizo,lakini haitoshi kuwa kipimo tosha na cha pekee kwa mtu aliyefanikiwa,kwa sababu ninachozingatia pesa na vitu inavyovinunua,sio muhimu sana,kilichokuwa ni muhimu je tunafanya mchango wowote katika jamii??
Mafanikio ya kimaisha yanamanisha kuweka zaidi katika maisha kuliko kuchukua,nafikiri mafanikio
yanavuka mipaka yetu wenyewe na kusaidia wengine katika njia mbalimbali.Hili linaweza kuwa rahisi,inaweza kuwa baba anayehamasisha watoto wake namna ya kutengeneza maisha yao yabaadae,au kwa mama anayeongoza watoto wake kuhusu imani juu ya Mungu,na wao kujiamini wenyewe.kwenye fikra zangu sina mashaka kuwa kama tutafanya kila kitu kwa kujiamini na kumtanguliza mungu utafanikiwa tu mimi nimekuwa shuhuda wa hilo,wote wanaojiamini na kupenda wanachokifanya wanafanikiwa zaidi,kwani mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya na sio kufanya unachokipenda.

KIPAJI,suala jengine huwa ni kipaji,nimewasikia watu wengi wakisema,nilipokuwa nazungumzia habari ya kipaji oh...bahati mbaya mimi hakunijalia kipaji kabisa,hilo sio la kweli kila mtu mungu ameumba na kipaji cha kipekee,unachotakiwa ni kufanya kadiri uwezavyo ili ubaini kipaji chako,tatizo la sasa kila kijana anataka kuwa mwanamuziki hata kama kipaji hana,au anataka kuwa mchezaji mpira achezee timu ya taifa au klabu kubwa kubwa tu,wanasahau kuna fani nyingi zipo na kama unachokipaji cha kweli unaweza kufanikiwa maisha hata kwa upande huo mwingine,kugeza talanta ya mwenzako kunaua kipaji chako na kunaweza kukufanya usifanikiwe kumbuka kuna kitu mungu amekupatia cha kipekee ambacho unaweza kukifanya ukamzidi hata huyo unayemgeza...




INAENDELEA WIKI IJAYO....

PIGA 0656538476 KWA MATANGAZO.

0 Response to "FIKIA MAFANIKIO YAKO SASA.W"

Chapisha Maoni