ZA UKWELI SANA

CHAMELEONE AMLILIA MR NICE.

  Mwanamuziki josee chameleone wa nchini uganda,ambaye ameweka heshima nchini kwake na Afrika mashariki kwa ujumla,kwa kushinda tuzo mbali mbali,na kuwa ni moja ya wasanii waliokaa kwa muda mrefu  katika chati mbalimbali na kuwa ni miongoni mwa wasanii wenye kipato kikubwa afrika mashariki.jana msanii huyo aliandika katika mtandao wake wa instagram kwamba amesikitishwa sana na habari alizozipata kuhusu ugonjwa wa mr nice na amuombea mungu aweze kupona kwa haraka sana,mr nice alilazwa hospitali kwa wiki mbili baada ya kudaiwa kupewa sumu,wakati akimfanyia kampeni mbunge wa kahama kwa tiketi ya chadema bwana james lembeli.
     namshukuru mungu na yesu kristo wa nazareti pamoja na familia yangu kwa ujumla kwa kuwa nami kipindi chote cha kuugua kwangu,jamani uchaguzi huu ni wa kupita,tusijengeane chuki kisa eti msanii fulani anampigia kampeni mgombea mwingine ambaye wewe humpendi,unataka kumuua mwenzako kisa kampeni lakini mungu ni mwema namshukuru mungu naendelea vizuri,nawaomba waandishi wa habari msinitafute wala kunipigia simu kwa sababu sipendi kiki kupitia matatizo.aliandika hivyo nice lucas mkenda kupitia mtandao wake wa facebook.
mr nice
mungu akuponye mr nice.

0 Response to "CHAMELEONE AMLILIA MR NICE."

Chapisha Maoni