ZA UKWELI SANA

TUSIJIFUNZE KWA WALIO SHINDWA.

Mpendwa nilikuwa nikijiuliza kila siku kwamba kila mtu katika maisha,anataka kutimiza ndoto zake katika maisha,na kufanikiwa katika mambo kadha wa kadhaa,lakini ili ufanikiwe ni lazima tujifunze kwa watu ambao,tumeona wamefanikiwa kwa namna moja au nyingine,kwa kuomba ushauri na hata kusoma na kufuatilia njia walizopitia,epuka ndugu yangu kujifunza kwa watu walioshindwa kwani wengine watakukatisha tamaa,watakupa ushauri usiofaa na wengine kwa roho zao nyeusi watataka uwe kama wao,si unajua tena roho ya mwafrika na hasa mbongo.

hawa ni baadhi ya watu ambao tunaweza kuwasoma kuwafuatilia na kujifunza kupitia wao wapo wengi lakini hawa ni baadhi yao tu,tutakuwa tukikushua na wengine kila tutakapo jaaliwa.
steven kanumba the great,steve biko huyo ni mwanaharakati wa south afrika alikuwa akipigania uhuru wa mtu mweusi,na chinua achebe  mwandishi wa vitabu wote ni marehemu kwa sasa kwangu ni mfano wa kuigwa.

0 Response to "TUSIJIFUNZE KWA WALIO SHINDWA."

Chapisha Maoni