ZA UKWELI SANA

HUYU NI MTOTO WA AJABU ZAIDI DUNIANI.

Kipaji cha mtoto huanza kuonekana taratibu wakati anaendelea kukua,mara nyingi wazazi huwa wanakuwa wa kwanza kutambua mwanawe anataka nini kwa maisha yake ya baadae lakini kipaji cha mtoto Esther Okode kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja
unaweza usiamini lakini huu ni ukweli,Ester ambaye ana umri wa miaka 10 na amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha uingereza miezi mitatu iliyopita na kudahiliwa asome masomo ya shahada ya hesabu.

Mtoto huyo ambaye ametokea katika mji wa waslaw, uliopo Midlands,uingereza sio mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake,mdogo wake wakiume mwenye miaka sita anasoma masomo ya  kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
Pamoja na Ester kudahiliwa miezi 3 iliyopita anaonekana kufanya vizuri kuliko wenzake darasani.

Mama yake Ester aitwaye Ife amesema kitendo cha mwanawe kujiunga na chuo kikuu kimewashangaza wengi,kutokana na umri wake lakini mwenyewe anajiamini

source millardayo.com

0 Response to "HUYU NI MTOTO WA AJABU ZAIDI DUNIANI."

Chapisha Maoni