ZA UKWELI SANA

MACELEBRITIES WA KIBONGO NA SHOW ZAO ZA TV..

mpendwa msomaji wa makala hizi za hoja kuntu,zinazokujia kwako kila jumanne na ijumaa,ninayofuraha kubwa kukaribisha tena leo kwenye mada hii ya leo ya macelebrities wa kibongo na show zao za tv nadhani si jambo geni sana siku hizi hapa bongo mastaa wengi wamekuwa wakianzisha show za television,kwa kweli hatujapata wasaa wa kukaa ana kwa ana na mastaa hawa kuhojiana ni kipi hasa kilichowapelekea kuanzisha show hizo lakini nadhani hata tukiwafanyia mahojiano majibu tutakayoyapata yatakuwa ni kwa ajili ya commercial purpose,kupata matangazo na kuendelea kujibrand zaidi na zaidi ni sawa tu,lakini nimekuwa nikijiuliza kila siku baadhi ya show ninazoziona kwa baadhi ya celebrities hawa zimekuwa hazina positive impact kwa jamii zao ambazo nyingi ni hali za chini kabisa na tabaka la kati ambao ninaamini wao kwa namna moja au nyingine ndio wamewafanya wao kuwa hapo.
kwa mfano show ya Diary ya lady jay dee,mwanadada nguli wa muziki wa bongo fleva hapa bongo,nadhani ni mtu mwenye heshima kubwa sana hapa bongo,kwa kazi zake anazofanya na tunampongeza sana,lakini nimekuwa nikiitazama ile show yake nimekuwa sipati majibu sawa sawa kabisa,show inaweza kuanza anaonekana amelala,mara kaamka anaonekana anamchemshia mbwa kilo mbili za supu tena nyama safi iliyonona kabisa,hivi najiulizaga ameshawahi kukaa na kujiuliza ana jua maisha wanayoishi mashabiki wake kuna watu wanakata mwaka hawajasikia harufu hata ya mchuzi,leo hii unatumia saa moja nzima kutuonyesha maisha yako ya kifahari  unayoishi,sikatai au sijasema kwamba jide hatoi miaada hapana,nadhani angetumia platfom kubwa kama kuwasaidia watu,kuwanyanyua vijana kisanaa,kuna watu wanahitaji laki mbili tu za matibabu hawana wewe leo unafanya israfu kwa kuuonyesha ulimwengu.




sawa mnaweza kusema anasaidia ila hapendi kujionyesha,hivi mna fahamu kuna wata wana matatizo lakini hawawezi kumface moja kwa moja na kumuelezea kwani hawajui waanzie wapi na waishie wapi lakini utakapo tangaza kwenye tv kama vile na kuweka namba za simu utawasaidia wengi,nakuwaambia utawasaidia vipi na wakupate wapi,wema sepetu ni kucheka cheka,kunongonezana na martin kadinda na  kutonyesha bithday zenu ni sawa hatukatai lakini mnayajua maisha ya watanzania wenzenu,tupendane sidhani ni jambo la kujivunia sana kuonyesha ufahari kwenye tv wakati ukienda posta watoto kibao wanaomba omba,mtasema hata ulaya wanafanya hali za kiuchumi za ulaya na marekani huwezi fananisha na bongo  kabisa.
oprah winfrey ni mwanamama tajiri sana lakini hafanyi show za kipuuzi kama hizo,show yake imempa umaarufu na imesaidia watu wengi sana duniani kwanini tusiige huu mfano kuliko kutafuta pesa na sifa ambazo utakufa utaacha hapa duniani.
tunampongeza sana mwanadada mboni wa the mboni show,show yake ni nzuri sana,ina elimisha,inahamasisha vijana na mara nyigine imewasaidia hata wagonjwa na wanafunzi wenye mahitaji ya kimasomo,hata mwaka jana alipata ajali akitokea Dodoma kusaidia jamii,na akampoteza director wake marehemu George Tyson,mungu ailaze pema roho yake,Mboni Masimba anasitahili sana pongezi na ni mfano wa kuigwa.
mwanadada sporah wa the sporah show,pia tunampongeza show yake inawahamasisha vijana sana kwa kuwajua mastaa duniani kote,jamani tubadilike hatuna chuki na mtu,lakini tubadilike tuache upumbavu na mambo ya kuiga toka ulaya,kabla sijamaliza nataka kumpongeza dada irene uwoya,show yake ya nyumba ilikuwa nzuri sana ila hatujui amekwamia wapi ila tumpongeza na kumtia moyo,tubadilike wabongo wenzangu,tukumbuke nchi yetu ni masikini sana.




tuwasiliane hapa.

0656538476.
 

0 Response to "MACELEBRITIES WA KIBONGO NA SHOW ZAO ZA TV.."

Chapisha Maoni