ZA UKWELI SANA

WATOTO WOTE NI WA KWETU MITAA HAINA WATOTO.

Mpenzi msomaji wa blogu hii pendwa,kila siku nakaa nakujiuliza hivi watoto wa mitaani chanzo na asili yake ni wapi maana kila siku wanaongezeka hasa katikati ya miji na majiji makubwa,je hawana wazazi,ni moja ya maswali pia ninayojiuliza lakini nakuja kugundua kuwa hawa watoto wanazaliwa na baba na mama mmoja lakini wazazi wa hawa watoto huwatelekeza watoto hawa au huwa wamefariki kwa maradhi,ajali na mambo yanayofanana na hayo,lakini je sisi kama jamii yaani mimi na wewe tunachukua hatua gani kupunguza hawa watoto wa mitaani au kuwasaidia kwa namna moja au nyingine kwa maana hawa nao ni watoto na wanahitaji huduma muhimu kama malazi,chakula,elimu na kupendwa na kuthaminiwa pia kama watoto wengine,je tunajenga taifa gani baadae,hayo ni maswali mengine tunatakiwa kuwaza zaidi,kweli nchi hii ina matajiri,viongozi wakubwa na watu wenye uwezo kweli tunashindwa kuwasaidia hawa,je wizara inayohusika na watoto inatengewa mabilioni kila mwaka yanakwenda wapi,je nyie wazazi mnaotelekeza watoto kwa nini mnajizalia kama hamjajipanga.
ok;jamani nadhani si muda wa kulaumiana,kusaidia si utajiri ila inahitaji utajiri tu wa imani,nyie mapedeshee mnatupa mahela mangapi huko kwenye mabar ili muimbwe na maband kutafuta sifa,halafu likiongozi jengine linajidai linajivuni nchi yake,huku linafurahi kuwaona watoto wakiomba omba barabarani,jamani hii haipo sawa na haipendezi,hawa watoto ndio taifa la kesho je watoto wenu mnaowasomesha ulaya,unadhani watakuwa na love na hawa machokoraa,je hamjafikiria tu panya road wanatoka wapi na ni wakina nani mpaka sasa,panya road ni chokoraa aliyekomaa.
jamani tuwe na roho ya imani mtoto wa mwenzio ni wako,je mnadhani hawa madogo watakuwa wazalendo na nchi yao kwa hali kama hiyo mnayoiona hapo,haihitaji pesa nyingi kubadilisha hiyo hali,inahitaji utajiri wa imani tu.


tuwasiliane hapa kama umeguswa au tuma ujumbe mfupi.
0656538476.
 

0 Response to "WATOTO WOTE NI WA KWETU MITAA HAINA WATOTO."

Chapisha Maoni