ZA UKWELI SANA

ARSERNAL YAFANYA MAUAJI KWENYE EPL.

Washika bunduki toka jijini london arsenal,jana wamefanikiwa kuwafunga aston villa kwa ushindi mnono wa 5 kwa 0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa emirates katika mwendelezo wa ligi kuu england.


arsenal walianza mchezo huo wa kasi wakifunga bao la haraka kwenye dakika ya 8 mfungaji akiwa mshambuliaji raia wa ufaransa olivier Giroud baada ya pasi ya beki per Mertersecker.

arsenal walifunga bao la pili kupitia kwa kiungo mshambuliaji mesut ozil ambaye alipokea pasi kutoka kwa Giroud na kuukokota mpira kabla ya kupiga shuti dogo lililompita kipa wa aston villa Brad Guzan.

Theo wallcot aliifungia arsenal bao la tatu kwenye dakika ya 63 baada ya kupewa pasi na santi cazorla ambaye alikuwa mmoja kati ya wachezaji walio shine katika mchezo wa jana.

bao la nne lilifungwa kwa njia ya penati baada ya kipa wa aston villa brad guzan kumchezea vibaya mshambuliaji chipukizi chupa akpom,sant cazorla alipiga penati hiyo na kuipa timu yake bao lingine huku aston villa wakiendelea kupata wakati mgumu.

wakati mchezo ukielekea mwishoni,beki wa kushoto Hector Betlern alifunga karamu ya mabao baada ya kuipa arsenal bao la tano.

ushindi huu unawafanya arsenal kuchupa hadi nafasi ya tano wakiwa na point 42,point moja nyuma ya man united walioko nafasi ya nne.

0 Response to "ARSERNAL YAFANYA MAUAJI KWENYE EPL."

Chapisha Maoni