ZA UKWELI SANA

MWANABLOGU TAABANI BAADA YA KICHAPO...........

SAUDI ARABIA imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu RAIF BADAWI,kwa sababu ya afya yake.Mwanablogu huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha FORUM LIBERAL SAUDI ARABIA NERTWORK,ambao sasa umefungwa na serikali,alitarajiwa kuchapwa viboko 50 baada ya sala ya IJUMAA mapema hiyo jana.
          Mwezi mei mwaka jana,alihukumiwa miaka10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1000,kwa kutusi dini ya kiislamu pamoja na kutotii sheria.Bwana BADAWI alipokea awamu ya kwanza ya viboko ijumaa iliyopita huku kesi yake ikisababisha tuhuma nzito kwa jamii ya kimataifa dhidi ya serikali yake ya saudia .Hata hivyo serika   haikutoa tamko lolote kwa kukosolewa,kadhalika,serikali haikutoa tamko kuhusu afya ya mwanablogu huyo,napia kuhusu kuahirishwa kwa adhabu yake.
 pichani mwanablogu RAIF BADAWI 
   PICHANI WANANCHI WANAOMUUNGA MKONO BADAWI WAKIWA NA MABANGO.                                                                                                                                               

0 Response to "MWANABLOGU TAABANI BAADA YA KICHAPO..........."

Chapisha Maoni