ZA UKWELI SANA

MALI ZA KOMBA KUPIIGWA MNADA

Mali za mbunge wa mbinga magharibi,kapteni john komba zimetangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa,kulipa deni analodaiwa na benki ya CRDB,mali hizo  zinahusisha eneo lenye ukubwa wa mita 2,214 liliopo Mbezi Tangi bovu,Daressalam kiwanja namba 1030kilichosajiliwa kwa jina la john Damiano Komba na Salome Komba.kwa mujibu wa tangazo,lililotolewa  kwenye vyombo vya habari,na kampuni ya uwakili ya Mpoki and associates Advocates inayowakilisha CRDB imetangaza kuuza eneo hilo,la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta,maduka makubwa,benki,sehemu ya kufanyia mazoezi,hospitali na huduma nyingine za kijamii.Tayari eneo hilo lina nyumba kubwa ya kuishi,upande unaotazamana na barabara ya Bagamoyo na kwa upande wa kusini mwa jengo kuu linalotazamana na barabara hiyo kuna nyumba nyingine ya kuishi,fremu za maduka na ofisi ilisomeka sehemu ya tangazo hilo.Alipoulizwa gharama halisi anazodaiwa kapteni komba na muda wa deni hilo,mmiliki wa kampuni ya Mpoki and advocates inayoratibu mnada huo,Mpale Mpoki amesema CRDB wanaweza kujibu hilo.

0 Response to "MALI ZA KOMBA KUPIIGWA MNADA"

Chapisha Maoni