ZA UKWELI SANA

JARIBU KUWA WEWE KATIKA MAISHA.

        Ndugu msomaji wa blog hii ya jicho la kitaa ninayofuraha kubwa ya kipekee kukaribisha katika makala hii ya leo katika kipengele hiki cha Hoja Kuntu,natumaini wote mtakuwa hamjambo kwa uweza wake wa kipekee bwana wa viumbe vyote,poleni sana na uchovu wa wiki nzima katika utafutaji wa riziki,kama mada inavyojieleza hapo juu leo baada ya kutafakari nikaamua kukuletea suala hili,mbele ya macho yako.Kiukweli kila mtu ana namna yake ya kufikiri na kutenda mambo,huko nchini marekani kulikuwa na mchungaji mmoja na kanisa lake lenye waumini wengi sana,na alisifika kwa namna alivyokuwa akitenda miujiza na mkono wa mikono Mungu kweli ulikuwa juu yake,lakini mchungaji yule ilifika hatua alikuwa mzee sana na hatimaye alifariki.akaulizwa mtoto mmoja wa kiume aliyekuwa karibu na marehemu baba yake je angeweza kuvaa viatu vya baba yake,alijibu hapana nisingeweza kuvaa viatu vya baba yangu,bali akajibu atavaa viatu vyake yeye mwenyewe na akakabidhiwa kanisa, na baada ya miaka kadhaa kanisa likawa kubwa saana kuliko  baba yake,na akafungua matawi marekani nzima.Huu ni mfano mzuri saana wa kuigwa ni lazima tuwe halisi na tujifunze kuwa sisi kama sisi,kama wewe ni mfanya biashara jaribu kuwa mbunifu na fanya mbinu za kukufanikisha kwa kujifunza zaidi,sio hapa panauzwa mihogo na wewe uuze mihogo,nimeona wachekeshaji wengi bongo wanaiga staili zilezile  walizotumia kutoka nazo wenzao,au wanamuziki wa kuimba yaani wanakopi kila kitu bila hata kubadili kidogo,kuiga sio vibaya lakini weka utofauti kidogo angalau iwepo tofauti kati yako na yake,kuwa wewe kama wewe,hata katika maisha usitamani maisha ya mwenzako kwani kila mtu ana njia zake,na jinsi mungu alivyo mjalia,huwezi kuwa mtu mwingine wewe ni wewe,na yeye ni yeye mwisho tukumbuke kukopi sio mbaya ila tusigandamizie wadau,tutaumia......lazima tujue kutofautisha kati ya msalaba na jumla,x na kuzidisha kama kijana wangu diamond alivyosema,jaribu kuwa original na usifeki mtu wangu wa nguvu.mimi na wewe tukutane next week mungu akipenda kwa leo ni hayo tu piga simu hii kwa ushauri swali au lolote  0656538476.

0 Response to "JARIBU KUWA WEWE KATIKA MAISHA."

Chapisha Maoni