ZA UKWELI SANA

MZEE WA UPAKO(TB JOSHUA MBABAISHAJI)

       Mchungaji wa kanisa la Maombezi liliopo maeneo ya Ubungo kibangu RGC (Tutashinda) mchungaji Antony Lusekelo leo katika Ibada alipokuwa akitoa mahubiri yake alisema nakusisitiza tena kwamba TB joshua nabii na Mhubiri wa Kimataifa Kutoka nchini Nigeria,ni nabii wa uongo na nitapeli tu kama alivyosema hapo awali.
    "Huyu jamaa ni muongo na tapeli tu ndio maana mungu amemuumbua jengo lake la kanisa limeanguka na kuuwa watu zaidi ya 100,kama yeye ni nabii wa ukweli mbona asitabiri kuhusu jengo lake ili awaepushe watumishi wake na vifo?
   "eti alikuwa anaoga ukiwa unaoga ndio ushindwe kujua kitakachotokea?mbona anawatabiria wenzake sijui ndege itapotea,sijui utashinda uraisi hamna kitu ana buni buni tu,hata mseme namponda sawa lakini hiyo ndio injili,mnadai kazi yangu kuponda wenzangu,kuna watu walimfuata mke wangu kwa maana wanajua mi siingiliki,wakamwambia eti hivi karibuni nitakufa kifo cha mwili kabisa nikaawambia mimi sifi wataanza kufa wao kwanza kwa jina la yesu mimi naongea ukweli tu na ndiyo injili hiyo.
  

Katika hatua nyingine mzee wa upako amewashauri waumini wake wa kanisa hilo kula matunda sana kwani ni safi kwa afya zao,wasisubiri mpaka waumwe tu,matunda yanaepusha magonjwa pia.

0 Response to "MZEE WA UPAKO(TB JOSHUA MBABAISHAJI)"

Chapisha Maoni