ZA UKWELI SANA

GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME WA MAJUMBANI BURE KUANZIA MWAKANI.

Gharama za kuunganisha umeme wa majumbani zitatolewa bure kuanzia mwakani mwezi machi baada ya ujenzi wa bomba la gesi kukamilika kutoka mtwara hadi Dares salaam kukamilika kwa asilimia 90.
          Aidha gharama za matumizi ya umeme wa majumbani na viwandani zitapungua kwa kiasi kikubwa baada ya mtambo huo  kuanza kufanya kazi.
    Msemaji mkuu Wizara ya Nishati na Madini,alisema hayo jana alipotembelea mtambo huo Kinyerezi akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dares salaam Ramadhani Madabida,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Waandishi wa Habari,Alisema kuwa gharama za watumiaji wa umeme kwa Tanzania ziko chini kwa asilimia tano ukilinganisha na nchi za Uganda asilimia(24) na Burundi asilimia (20)
   "Mtambo wa kusafirishia Umeme wa gesi ambao ukubwa wake ni kama ule wa Ubungo umekamilika kwa asilimia 90.
  Alisema kuwa serikali imeajiri wafanya kazi waTanzania kwa asilimia 95.
Na ifikapo January vijana asilimia 60,watapelekwa nchini China kwa masomo ili wapate ujuzi wa kuendesha mitambo hiyo.
Mhandisi anaye simamia mradi huo Saimon Gilma,alisema mradi huo umetumia Dola za Kimarekani milioni 103,ambazo zote zimelipwa na Serikali ya Tanzania.
      Alisema ujenzi wa miundo mbinu ya mitambo hiyo imekamilika kinachosubiriwa ni kuletwa kwa mitambo hiyo kutoka bandarini.
     Aidha za nyumba za wafanyakazi,watakaoendesha mitambo hiyo zimekamiliks kwa ajili ya kuanza kazi,alifafanua kuwa mabomba ya gesi yaliyo tandazwa ardhini kutoka Mtwara hadi Dare es Salaam ni transfoma 200 na yatawekewa ulinzi mkali Ikiwa ni Pamoja na Helkopta itakayokuwa inazunguka usiku na mchana.

      Alisema kuwa gharama za kuweka umeme nyumbani zitagharamiwa na nchi ya Japan na Finland,wananchi watatakiwa kutoa sehemu ya Viwanja vyao au mashamba ili kupisha bomba hilo Kupita.

0 Response to "GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME WA MAJUMBANI BURE KUANZIA MWAKANI."

Chapisha Maoni