ZA UKWELI SANA

Wilaya ya Muheza mkoani Tanga walia na Shida ya Maji.

Tanga.
    Wakazi wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga wamelalamikia tatizo la maji wilayani humo lilodumu kwa muda mrefu,wamesema miundo mbinu iliyopo sasa haitoshi kabisa kukidhi mahitaji ya maji wilayani humo.
  Akizungumza kwa jaziba mwenyekiti wa kijiji cha Genge wilayani humo amesema maji kwa sasa kijijini humo yanatoka kwa mgawo ambapo wanaweza kukaa mfululizo wa wiki mbili bila kupata maji,amesema kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita changamoto hiyo ya maji haikuwepo kabisa lakini hivi sasa kutokana na kukua kwa mji na kuongezeka kwa wakazi huku miundo mbinu ikibaki ile ile.
  Lakini wamelalamika kwamba Tanga mjini kwenye wakazi wengi hakuna kabisa shida ya maji,na chanzo kikuu kikiwa mto Zigi kiliopo hapo wilayani Muheza.
  Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake kijana mmoja wilayani humo amesema licha ya ahadi kedekede za viongozi wilayani humo kwa kila vipindi vya uchaguzi hakuna lolote linalofanyika .
  Wakazi hao wamesema wanaomba serikali iwakumbuke na kuwaacha kuwafanya watoto wamechoka na ahadi za uongo.

0 Response to "Wilaya ya Muheza mkoani Tanga walia na Shida ya Maji."

Chapisha Maoni