ZA UKWELI SANA

Watanzania watatu wakutwa na hatia ya Kula Njama Kumuua Mkuu wa Zamani wa Majeshi Ya Rwanda.

  Watanzania watatu,Hemedi Dendengo Sefu,Hassani Mohamedi Nduli na Abdou,jana walitiwa hatiani na Mahakama moja nchini Afrika Kusini kwa kosa la kula njama za kumuua aliyekuwa mkuu wa Majeshi ya Rwanda Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa mwezi juni mwaka 2010.
      Watanzania hao walikuwa Miongoni mwa watuhumiwa Sita,ambao wawili walikuwa hawana hatia,na mmoja,raia wa Rwanda,alitiwa hatiani,watahukumiwa mapema mwezi ujao.
    Hakimu Aliendesha kesi hiyo alisema kuwa lengo la Mauaji hayo ni la kisiasa.Jenerali Kayumba alikimbilia uhamishoni Afrika kusini baada ya kutibuana na rafiki yake wa zamani raisi wa sasa wa Rwanda Paul Kagame.
  Hata hivyo,Rwanda imekanusha kuhusika na mpango huo wa mauaji hayo.
     Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC)alieleza kuwa Mkuu huyo wa zamani wa majeshi ya Rwanda alikuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo inatolewa.
  "Mahakama imeeleza kwa usahihi kuwa mpango wa kuniua ulikuwa wa kisasa zaidi"alisema Nyamwasa .
   Mmoja wa watanzania hai,sefu alitajwa kuwa ndiye aliyepangiwa Kumpiga risasi Jenerali huyo.

0 Response to "Watanzania watatu wakutwa na hatia ya Kula Njama Kumuua Mkuu wa Zamani wa Majeshi Ya Rwanda."

Chapisha Maoni