ZA UKWELI SANA

Mahabusu wanyanyaswa na kulawitiwa mahabusu.

Mahabusu hao wanaozuiliwa huko Daresalam wanadai kuhojiwa wakiwa uchi wa mnyama kulawitiwa na askari wa jeshi la polisi,kuwekewa vitu vyenye ncha kali kwenye sehemu za haja kubwa na mateso mengine mengi ikiwa ni pamoja na kupigwa hadi kuumizwa.
Hata kama ni wakosaji wa matendo hayo ni kinyume na haki za binadamu hayapaswi kufanyiwa binadamu kama hawa tena raia halali wa Nchi hii.
Tunauliza ipo wapi haki ya kisheria ya Mwananchi wa nchi hii ikiwa jeshi la polisi ndio wanaovunja sheria badala ya kulinda?
  Inashangaza kuona vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Makaburu dhidi ya watu weusi wa Afrika kusini sasa vinafanywa na vijana wa Tanzania dhidi ya watanzania wenzao kwa kisingizio cha ugaidi.
  Sisi Cuf hatuoni mantiki ya uvunjaji wa Haki za binadamu kiasi hiki kwa watu wanaotuhumiwa kwa kile kinachoitwa kujishirikisha na matendo ya kigaidi.
Chama cha Wananchi Cuf kinawaomba ndugu na jamaa pamoja na waislamu wote nchini kuendelea kuwa na Subira tukiamini kwamba sheria itachukuliwa dhidi ya viongozi hawa.
     Imetolewa na Abdul Kambaya
        Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Cuf.

0 Response to "Mahabusu wanyanyaswa na kulawitiwa mahabusu."

Chapisha Maoni